Mamlaka ya Uturuki imemzuilia Lorenzo Prendini, msimamizi Mmarekani wa jumba la makumbusho, mjini Istanbul kwa madai ya kujaribu kusafirisha viumbe vyenye sumu kutoka Uturuki.
Polisi wa Istanbul walipanga operesheni siku ya Jumatatu katika uwanja wa ndege wa Istanbul baada ya kugundua jaribio la kusafirisha viumbe hao nje ya nchi.
Prendini alikamatwa na mzigo wenye wadudu wanaopatikana Uturuki, wakati wa operesheni hiyo chupa 88 za mirija ya plastiki zilizokuwa na vimiminika, na mifuko 58 iliyo na takriban nge 1,500, buibui mkubwa mwenye sumu (tarantula) na buibui.
Mshukiwa, mwangalizi wa Jumba la Makumbusho la Marekani la Historia ya Asili , anakabiliwa na mashtaka chini ya sheria ya Uturuki ya kupigana na magendo.
Ripoti za DNA za spishi za wanyama wenye sumu wanaoishi Uturuki zinaweza kutumika kutengeneza dawa.
Inakadiriwa kuwa lita 1 ya dawa inayotokana na sumu ya nge ina thamani ya karibu dola milioni 10.


















