Blinken awataka maofisa wa Israeli kujadili pendekezo la usitishwaji wa mashambulizi Gaza
Vita katka eneo la Gaza vimeingia siku ya 241 vikiwa vimeua Wapalestina 36, 439, asilimia 71 ikiwa ni wanawake, watoto wadogo na kujeruhi wengine 82, 627, maofisa wamesema.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, mwezi Oktoba. / Picha: Reuters / Others
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewataka maofisa wa Israeli kujadili pendekezo la makubaliano katika eneo la Gaza, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema.
Blinken alizungumza na Waziri Benny Gantz na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, kulingana na taarifa hiyo.
Katika mazungumzo hayo, Blinken "aliipongeza" Israeli kwa pendekezo hilo, kama lilivyobainishwa na Rais wa Marekani Joe Biden, na kwamba, jukumu sasa lilikuwa kwa Hamas ili wakubaliane nalo.