| Swahili
AFRIKA
3 DK KUSOMA
Malawi: Jeshi laendelea kuitafuta ndege iliyombeba Makamu wa Rais
Ndege hiyo ya kijeshi iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais Saulos Chilima, na mke wa zamani wa Rais, Shanil Dzi mbiri na watu wengine nane iliondoka kutoka uwanja wa ndege wa mjini Lilongwe saa tatu asubuhi ikitarajiwa kutua ndani ya dakika 45.
Malawi: Jeshi laendelea kuitafuta ndege iliyombeba Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Chilima./Picha: Reuters / Others

Wanajeshi wa nchini Malawi wanaendelea kuitafuta ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo iliyopoteza mawasilino na rada siku ya Jumatatu, Rais Lazarus Chakwera amesema.

Ndege hiyo ya kijeshi iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais Saulos Chilima, na mke wa zamani wa Rais, Shanil Dzi mbiri na watu wengine nane iliondoka kutoka uwanja wa ndege wa mjini Lilongwe saa tatu asubuhi ikitarajiwa kutua ndani ya dakika 45.

Hata hivyo, idara ya udhibiti wa anga iliitaka ndege hiyo kusitisha zoezi la kutua na kugeuza kutokana na hali mbaya ya hewa, alisema Rais Chakwera katika hutoba yake kwa taifa.

Kitengo hicho kilipoteza mawasiliano na ndege hiyo na ikatoweka kwenye rada muda mfupi baadaye, alisema.

“Najua hili ni jambo la kushtua kidogo. Najua sote tuna uoga na wasiwasi.

Hata mimi nina hofu,” alisema Chakwera . Lakini naomba niwahakikishie kuwa tunafanya kila jitihad akuitafuta ndege hiyo kukiwa na matumaini ya kuwapata manusura.”

Mzuzu ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Malawi. Unapatikana katika eneo lenye milima na misitu mingi.

Chilima ni nani?

Chilima alijijengea jina katika nyanja ya kibiashara kabla ya kuingia kwenye siasa.

Mwanasiasa huyo mwenye miaka 51, amewahi kushika nafasi za juu kwenye makampuni makubwa kama vile Unilever na Coca-Cola.

Tovuti ya serikali ya nchi hiyo inamuelezea Chilima kama mchapakazi hodari mwenye shahada ya Uzamivu kwenye 'usimamizi wa maarifa'.

Kiongozi huyo aliahidi kuendeleza msako wa ndege hiyo hadi usiku na kuongeza kuwa mamlaka zilitumia minara ya mawasiliano kuitafuta ndege hiyo, ndani ya kilomita 10 kutoka eneo la mashamba.

Kulingana na Rais Chakwera, zoezi hilo la utafutaji linaongozwa na Jeshi la Ulinzi la nchini Malawi.

“Nimetoa maagizo kuwa utafutaji uendelee hadi ndege ipatikane,” alisema Chakwera.

Chakwera aliongeza kuwa Marekani, Uingereza na Israeli zimejitolea kusaidia zoezi la utafutaji wa ndege hiyo kutokana na teknolojia zao za kisasa, na kuonesha matumaini ya kupatikana kwa ndege hiyo.

Chakwera alisema Dzimbiri, aliyekuwa mke wa zamani wa Rais wa zamani Bakili Muluzi, alikuwa ni mmoja wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, wakielekea kuhudhuria mazishi ya waziri wa zamani.

pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Afrika Kusini yaomba utulivu kufuatia maandamano dhidi ya kusimikwa kwa 'Igwe' wa Nigeria
Rwanda ‘yahofia’ operesheni za DRC dhidi ya kikundi cha FDLR
Kenya yalipa ada ya Dola milioni 30 ya uenyeji wa AFCON 2027
Hasara ya mamilioni kufuatia ubomoaji katika soko kubwa zaidi la wazi la Gikomba Nairobi
Shabiki maarufu ‘Lumumba Vea’ akosa viza ya  kwenda kuishangilia DRC dhidi ya Jamaica
Mamlaka ya uchukuzi Kenya yazindua ukaguzi wa lazima wa afya kwa madereva ili kupunguza ajali
Tanzania yahimiza matumizi ya AI kuimarisha mtangamano na maendeleo EAC
Kundi lenye silaha limewaua watu wasiopungua 20 Jimbo la Plateau nchini Nigeria
Wafungwa wasiopungua 11 wafariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika jela DRC
Kagame awaamuru maafisa waandamizi wa serikali 'kusimama' wakati wa hotuba yake
Wadukuzi wadukua maombi ya kazi 450,000 nchini Afrika Kusini
Rais wa Misri asema ni Trump pekee anaweza kusimamisha vita, aonya kupanda zaidi kwa bei ya mafuta
Togo yatoa uzoefu wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele
Watu 15 wamefariki katika ajali ya barabarani mkoa wa kati Kenya
Mahakama kuu ya Jamhuri ya Congo imethibitisha ushindi wa Sassou Nguesso kwa awamu ya tano
Rwanda, Burundi wanagombana juu ya juhudi za rais wa zamani wa Senegal Sall kuongoza UN
Vifo kutokana na mafuriko nchini Kenya vyaongezeka hadi 108, polisi wasema
Majenerali wakuu wa Uganda wazuiliwa kwa madai ya ufisadi: ripoti
Eswatini yamrudisha nyumbani mwananchi wa Cambodia aliyefukuzwa kutoka Marekani
Waasi waanza kuondoka katika vijiji vya DRC ili kuhimiza amani