| Swahili
AFRIKA
1 DK KUSOMA
Houthi: Tulitumia 'silaha mpya' kuzamisha meli ndani ya Bahari Nyekundu
Mashambulizi ya Israeli katika eneo la Gaza yameingia siku ya 258 yakiwa yameua Wapalestina 37, 396, wengi wakiwa ni akina mama na watoto wadogo, na kujeruhi 85,523, huku zaidi ya watu 10,000 wakihofiwa kufukiwa na vifusi.
Houthi: Tulitumia 'silaha mpya' kuzamisha meli ndani ya Bahari Nyekundu
Kikundi cha Houthi kimeituhumu meli ya MV Tutor  kwa "kuzima kifaa chake cha utambuzi wakati inapita kwneye Bahari Nyekundu." / Picha: TRT World   / Others

Kikundi cha Houthi cha Yemen kimesema kuwa kilitumia "silaha mpya" wakati wa kuilenga na kuizamisha meli ya mizigo ya MV Tutor katika Bahari Nyekundu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kikosi cha jeshi cha kikundi hicho na kurushwa kwenye televisheni ya Al-Masirah kinachomilikiwa na Houthi.

Kulingana na taarifa hiyo, "silaha mbalimbali za kivita zilitumika kuilenga na kuzamisha meli ya Tutor".

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, "Tukio hilo lilitokea baada ya chombo hicho kinachomilikiwa na kampuni ya Ugiriki, kukaidi agizo la kutokuingia bandari ya Haifa."

Taarifa hiyo pia iliituhumu meli hiyo "kwa kuzima mfumo maalumu wa utambuzi wakati kinakatisha katika Bahari Nyekundu."

pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika