Kenya: Maandamano yaathiri upatikanaji huduma za intaneti

Kulingana na NetBlocks, taasisi inayoshughulikia mwenendo wa matumizi wa huduma za intaneti duniani, huduma hizo zimeathirika kutokana na maandamano yakiendelea kushika kasi nchini Kenya.

By Edward Josaphat Qorro
Mchoro unaoonesha mwenendo wa upatikanaji wa huduma za intaneti nchini Kenya./Picha: netblocks X / Others

Huduma za intaneti zimeripotiwa kuathirika nchini Kenya, kufuatia maandamano ya kupinga muswada wa fedha 2024.

Kulingana na NetBlocks, taasisi inayoshughulikia mwenendo wa matumizi wa huduma za intaneti duniani, huduma hizo zimeathirika kutokana na maandamano yakiendelea kushika kasi nchini Kenya.

Wakati huo huo, chombo cha habari cha KTN News cha nchini Kenya kimeripoti kupokea vitisho vya kufunga chombo kutokana na namna walivyoripoti maandamano na vurugu za kupinga muswada wa fedha wa 2024.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels