Maafisa wa Uturuki na Urusi wajadili kuhusu Syria mjini Ankara

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Nuh Yilmaz alikutana na Mwakilishi Maalum wa Urusi kwa Syria Alexander Lavrentiev mjini Ankara kujadili Syria.

By Yusuf Dayo
Nuh Yilmaz na Alexander Lavrentiev walibadilishana mawazo kuhusu Syria. / Picha: Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki / Others

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Nuh Yilmaz amekutana na Mwakilishi Maalum wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa Syria Alexander Lavrentiev mjini Ankara, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

Wawili hao walibadilishana maoni kuhusu Syria kwa ushiriki wa taasisi husika, iliandika kwenye X siku ya Jumamosi.

Hakuna taarifa zaidi juu ya mkutano huo iliyofichuliwa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels