Liverpool yaongoza Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Wolves

Nyota wa Misri, Mohamed Salah alifunga kwa mkwaju wa penati huku vijana wa Arne Slot wakishinda mechi tano kati ya sita kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

By Edward Josaphat Qorro
Mohamed Salah akifunga bao la pili dhidi ya Wolves./Picha: Getty / Others

Liverpool imechupa hadi kileleni mwa Ligi kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuifunga Wolves mabao 2-1.

Hata hivyo, 'majogoo hao wa Anfield' walipitia kipindi kigumu katika dakika 20 za mwanzo wa mchezo huo, baada vijana wa Gary O'Neil's kuwabana mabingwa hao wa zamani Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Hapo awali, timu ya Arsenal ilitoka nyuma na kufunga magoli mawili katika dakika za majeruhi dhidi ya Leicester City, na kisha kuibuka washindi kwa magoli 4-2 katika mchezo wa Ligi ya Uingereza (EPL).

Mchezo huo uliopigwa siku ya Jumamosi ndani ya dimba la Emirates jijini London, unawaweka ‘Washika Bunduki’ hao nafasi moja na Manchester City, wote wakiwa na alama 14 kila mmoja, baada ya michezo sita.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels