Idadi ya vifo nchini Lebanon yafikia 2,255 Israeli ikishambulia vijiji
Mashambulizi ya Tel Aviv dhidi ya Gaza yameua Wapalestina wapatao 42,175. Wakati huo huo, mashambulizi ya Israeli katika eneo la Lebanon yameua zaidi ya watu 2,169 na kuwakosesha makazi watu milioni 1.2 tangu Oktoba 2023.
Uharibifu mkubwa uliosababishwa na shambulio la anga la Israeli katika eneo la Nowayri mjini Beirut nchini Lebanon./Picha: AA / Others
Idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya Israeli nchini Lebanon imeongezeka na kufikia 2,255 huko majeruhi wakiwa 10,524, Wizara ya Afya ya Lebanon imesema.
Kulingana na Wizara hiyo, watu 26 wameuwawa na wengine 144 kujeruhiwa ndani ya saa 24.
Israeli imefanya mashambulizi makubwa ya anga kote Lebanon dhidi ya kile inachodai kuwa malengo ya Hezbollah tangu Septemba 23 ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya waathirika 1,437.