Wakenya wang'ara Chicago Marathon 2024

Mkenya Kelvin Kiptum pia aling'ara katika mbio hizo mwaka jana kabla ya kufariki dunia kwa ajali ya gari mwaka 2024.

By Edward Josaphat Qorro
Ruth Chepngetich wa Kenya ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Chicago Marathon 2024./Picha: Getty      / Others

Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepngetich amefanikiwa kuweka rekodi mpya duniani baada ya kumaliza mbio za Chicago Marathon ndani ya saa 2:09:57.

Mafanikio hayo yanamfanya Chepngetich kuvunja rekodi ya awali ya saa 2:11:53 iliyokuwa inashikiliwa na Tigst Assefa kutoka kwa Ethiopia.

Kwa upande wa wanaume, John Korir aliibuka shujaa baada ya kumaliza mbio hizo ndani ya saa 2:02:43, ambao ni ushindi wake mkubwa kwenye mashindano hayo.

Mkenya Kelvin Kiptum alishinda mbio hizo mwaka jana kabla ya kufariki dunia kwa ajali ya gari mwaka 2024.

Zaidi ya wanariadha 50,000 walishiriki mbio hizo zilizofanyika siku ya Jumapili katika mitaa ya Chicago nchini Marekani.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels