Eneo la Uturuki Mashariki lakumbwa na tetemeko la ardhi la ukubwa wa 5.9

Tetemeko kubwa lilitikisa eneo la Malatya Kale lililo mashariki mwa Uturuki siku ya Jumatano huku kukiwa hakuna taarifa zozote za vifo.

By Edward Josaphat Qorro
Eneo la Malatya lina historia ya mitikisiko ya aina hiyo huku idara za kukabiliana na majanga katika eneo hilo zikiwa tayari kukabiliana na dharura za namna hiyo./Picha: AA / Others

Tetemeko lenye ukubwa wa 5.9 limepiga eneo la Mashariki la Uturuki, huku chanzo chake kikiwa ni Malatya katika wilaya ya Kale, kwa mujibu wa Idara ya Kushughulikia Majanga ya Dharura nchini Uturuki (AFAD).

Tetemeko hilo, lililotokea majira ya saa 10.46 asubuhi siku ya Jumatano, lilianzia kwa ukubwa wa kilomita 10.07.

Taarifa za awali zinasema kuwa hapakuwa na ripoti zozote za vifo, ingawa uchunguzi zaidi unafanyika katika eneo la tukio, kwa mujibu wa meya wa Malatya, Sami Er.

Mamlaka zinaendelea kufuatilia tukio hilo kutathmini uharibu wowote uliojitokeza hasa katika maeneo ya kijijini ambako ndio kitovu cha tetemeko hilo. Mamlaka za uokoaji zimeendelea kuwa tayari kukabilina na hali hiyo, ili kuhakikisha kuwa watu wa eneo hilo wanaendelea kuwa salama.

Malatya ina historia ya mitetemo huku idara za kukabiliana na majanga katika eneo hilo zikiwa tayari kukabiliana na dharura za namna hiyo. Licha kutosababisha vifo vyovyote, wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa wameshauriwa kuchukua tahadhari.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels