Urusi kuchunguza kutunguliwa kwa ndege yake nchini Sudan

Ubalozi wa Urusi nchini Sudan umesema kuwa umeanza uchunguzi kuhusu ndege yao ya mizigo ambayo inadaiwa kutunguliwa huko Magharibi mwa Sudan.

By Edward Josaphat Qorro
Machafuko ya nchini Sudan yalianza katikati ya mwezi Aprili, 2023./Picha: AFP / Others

Ubalozi wa Urusi nchini Sudan umeanza uchunguzi wa madai ya kutunguliwa kwa ndege yake kaskazini mwa Sudan, umesema ubalozi huo siku ya Jumatatu.

Kulingana na ubalozi huo, ndege inaweza ikawa imetunguliwa na majeshi ya RSF, yanayogombania mamlaka nchini Sudan.

Kwa sasa, ubalozi huo, kwa kushirikiana na mamlaka za Sudan, unaratibu namna ya kupata taarifa zaidi, na kufahamu hatma ya waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels