Israel yawaua Wapalestina wasiopungua 62 kaskazini mwa Gaza

Vita vya mauaji ya halaiki ya Israel dhidi ya Gaza - sasa katika siku yake ya 389 - vimeua watu wasiopungua 43,020 na kujeruhi zaidi ya 101,110, huku wengine 10,000 wakihofiwa kufukiwa chini ya vifusi.

By Yusuf Dayo
Wakazi wanarejea makwao huku uharibifu mkubwa ukiachwa kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kutoka Beit Lahia, Gaza mnamo Oktoba 27, 2024. / Picha: AA / Others

Jumanne, Oktoba 28, 2024

0635 GMT - Shambulio la anga la Israel limepiga jengo la ghorofa tano la makazi huko Beit Lahia, kaskazini mwa Gaza, na kuua Wapalestina 62, na kujeruhi wengine 20, huku wakaazi kadhaa bado hawajulikani walipo, kulingana na wakala rasmi wa habari wa Palestina WAFA.

0324 GMT - Marekani, wakuu wa ulinzi wa Israel wanajadili suala la kupunguza mgogoro wa eneo

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Israel Yoav Gallant walikagua uvamizi wa kijeshi wa Israel na kujadili fursa za kupunguza uhasama katika kanda, Pentagon ilisema.

Katika mazungumzo ya simu na Gallant, Austin "alisisitiza kujitolea kwa Marekani kwa mpango wa kidiplomasia nchini Lebanon ambao unaruhusu raia wa Lebanon na Israel kurejea salama kwenye makazi yao pande zote za mpaka, pamoja na kuachiliwa kwa mateka na makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza. " alisema msemaji Meja Jenerali Pat Ryder katika taarifa.

Austin pia alithibitisha "msaada usioyumba" wa Washington kwa ulinzi wa Israeli.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels