Tanzania: Idadi ya vifo vilivyotokana na jengo kuporomoka yafikia 29
Vifo vilivyotokana ajali hiyo vimefikia 29, baada ya miili mingine tisa kupatikana wakati zoezi la uokozi likiendelea.
Idadi ya watu waliopoteza maisha katika tukio la kuporomoka jengo nchini Tanzania, sasa imefikia 29, serikali ya nchi hiyo imesema.
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Thobias Makoba, amesema kuwa shughuli nzima ya uokoaji katika eneo la soko la Kariakoo, imekamilika siku ya Novemba 26, huku idadi ya vifo vinavyotokana na tukio hilo la Novemba 16 ikifikia 29.
Hii ni baada ya kupatikana kwa miili mingine tisa, wakati wa zoezi la uokozi likiendelea, serikali hiyo imesisitiza.
“Kuanzia Novemba 26, eneo lote la Kariakoo linafunguliwa huku shughuli mbalimbali zikiendelea...isipokuwa eneo moja tu lililohusisha ghorofa kuporomoka ndilo litaendelea kufungwa kwa siku tatu kwa ajili ya kumalizia zoezi la uchunguzi,” alisema Makoba.