| swahili
UTURUKI
2 DK KUSOMA
Hakuna nguvu inayoweza kuwalazimisha Wapalestina kuondoka katika nchi yao
"Hakuna aliye na uwezo wa kuwaondoa watu wa Gaza kutoka katika nchi yao ya milele, Palestina, ikiwa ni pamoja na Gaza, Ukingo wa Magharibi, na Jerusalem Mashariki, ni mali ya Wapalestina," anasema Recep Tayyip Erdogan.
Hakuna nguvu inayoweza kuwalazimisha Wapalestina kuondoka katika nchi yao
Erdogan aliipongeza Hamas kwa kutimiza ahadi zake katika mabadilishano ya wafungwa yanayoendelea na Israel, licha ya majaribio ya Israel kuhujumu mchakato huo. / Picha: AA
10 Februari 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisisitiza tena kwamba hakuna nguvu inayoweza kuwalazimisha watu wa Gaza kutoka katika nchi yao "ya milele", kwani Gaza, Ukingo wa Magharibi, na Jerusalem Mashariki ni mali ya Wapalestina.

"Hakuna aliye na uwezo wa kuwaondoa watu wa Gaza kutoka katika ardhi yao ya milele, ambayo imekuwepo kwa maelfu ya miaka. Palestina, ikiwa ni pamoja na Gaza, Ukingo wa Magharibi, na Jerusalem Mashariki, ni ya Wapalestina," Erdogan aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumapili huko Istanbul kabla ya kuruka kuelekea Malaysia.

Mapendekezo ya utawala wa Marekani kuhusu Gaza, yaliyotolewa kwa shinikizo kutoka kwa utawala wa Kizayuni, hayafai kujadiliwa, alisema Erdogan, akizungumzia pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwahamisha Wapalestina.

Erdogan pia aliipongeza Hamas kwa kutimiza ahadi zake katika mabadilishano ya wafungwa yanayoendelea na Israel, licha ya majaribio ya Israel kuhujumu mchakato huo.

Kuhusiana na hali ya Syria, Erdogan alisema kwamba makaburi ya halaiki yanafukuliwa katika maeneo tofauti ya Syria, uso wa umwagaji damu wa utawala wa Assad unafichuliwa.

Rais wa Uturuki alielezea matumaini ya utulivu wa Syria chini ya uongozi wa Rais Ahmed Alsharaa, akipendekeza nchi hiyo itapata amani hivi karibuni.

Hakuna nafasi kwa makundi ya kigaidi nchini Syria, alisema Erdogan, akisisitiza kuwa Rais wa Syria Ahmad Alsharaa atapambana dhidi ya makundi hayo.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Wanajeshi 20 wa Uturuki wauawa katika ajali ya ndege ya shehena ya kijeshi huko Georgia: wizara
Ndege ya kijeshi ya mizigo ya Uturuki yaanguka mpakani mwa Georgia na Azerbaijan ikiwa na watu 20
Uimarishaji wa Uturuki ni heshima na kumuenzi Ataturk: Erdogan
Uturuki inamkumbuka Ataturk miaka 87 baada ya kufariki
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki kuzuru Marekani siku ya Jumatatu
Rais Erdogan anatumai Marekani itatimiza ahadi zake kuhusu makubaliano ya ndege za kivita za F-35
Palestina inapongeza amri za kukamatwa dhidi ya maafisa 37 wa Israel kutoka Uturuki kama 'ushindi
Ujumbe wa Erdogan 'Azerbaijan haiko peke yake' ulipelekea ushindi wa Karabakh: Aliyev
Ushindi wa Karabakh wa Azerbaijan kwa amani ya Caucasus: Rais Erdogan
Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu, juu ya mashtaka ya mauaji
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Uturuki kuandaa mazungumzo ya Gaza wiki ijayo kufuatia wasiwasi juu ya usitishaji mapigano – Fidan
Mfumo wa ulimwengu wa sasa unazingatia nguvu zaidi ya haki: Mkurugenzi wa TRT
Israel imeigeuza Gaza kuwa vifusi, inawezaji kuwa haina hatia: Erdogan
Uturuki yakashifu unafiki wa nchi za Magharibi kuhusu Gaza, yatoa wito wa mfumo mpya wa dunia
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Erdogan ataka kuona mabadiliko katika uhusiano na EU na ushirikiano wa kikanda alipokutana na Mertz
Ujerumani yatoa wito wa kuunda “ushirikiano wa kimkakati” ili kukabiliana na changamoto za kimataifa
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Erdogan ametangaza washindi wa Tuzo Kuu za Utamaduni na Sanaa za Urais mwaka 2025