| swahili
ULIMWENGU
4 DK KUSOMA
Adhabu ya kifo siyo sahihi katika karne ya 21 - UN
Mkuu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema mnamo 2023, watu 1,153 walinyongwa katika nchi 16 -- ongezeko la 31% kutoka 2022 na "idadi kubwa zaidi" katika miaka minane iliyopita
Adhabu ya kifo siyo sahihi katika karne ya 21 - UN
Umoja wa Mataifa unapinga aina zote za hukumu ya kifo,/ Picha: Getty 
26 Februari 2025

Mkuu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Jumanne alitoa wito wa kusitishwa na kukomeshwa kwa hukumu ya kifo, akionya kuhusu "ongezeko kubwa" la hukumu ya kifo duniani.

"Adhabu ya kifo ni jambo ambalo limepita na wakati na halifai katika karne ya 21. Wakati nchi kadhaa zinahoji kuwa iko ndani ya mamlaka yao ya kitaifa, kwa mtazamo wangu, haiendani na utu na za msingi za binadamu," Volker Turk alisema katika mjadala wa ngazi ya juu wa kila miaka miwili juu ya hukumu ya kifo chini ya kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva.

Akisisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unapinga aina zote za hukumu ya kifo, Turk alisema: "Ninasikitika sana kuripoti kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la hukumu za kifo duniani tangu tulipokutana mara ya mwisho miaka miwili iliyopita."

Mnamo 2023, watu 1,153 walinyongwa katika nchi 16 -- ongezeko la 31% kutoka 2022 na "idadi kubwa zaidi" katika miaka minane iliyopita, alisema. Hiyo ilifuatia ongezeko la asilimia 53 la watu waliouawa kati ya 2021 na 2022, aliongeza.

Nchi zinazoongoza kwa hukumu ya kifo

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa haki za binadamu, nchi zilizoongoza katika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na Iran, Saudi Arabia, Somalia na Marekani.

Alisema takwimu hizo hazijumuishi China, ambako taarifa hazipatikani kwa urahisi na hakuna uwazi kuhusu hukumu ya kifo.

"Ninatoa wito kwa mamlaka ya China kubadili sera hii na kujiunga na kauli ya kutaka kukomesha," alisema.

40% ya mauaji yanayohusiana na dawa za kulevya

Zaidi ya asilimia 40 ya mauaji haya -- idadi kubwa zaidi tangu 2016 -- ni ya makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, Turk alisema, akisisitiza kwamba idadi hii pia imeongezeka sana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, na karibu mauaji haya yote yalifanyika nchini Iran.

"Makosa yanayohusiana na dawa za kulevya hayafikii kiwango kilichowekwa na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, ambayo inahusu tu uhalifu mkubwa zaidi, unaohusisha mauaji ya kukusudia," alisema.

Mkuu huyo wa haki za binadamu pia aliangazia kasi inayokuwa kuelekea kukomesha hukumu ya kifo duniani.

"Ikipingana na ongezeko la kunyonga watu, kuna idadi kubwa na inayokua duniani dhidi ya hukumu ya kifo," alisema, akibainisha kuwa nchi 113 zimekomesha kikamilifu adhabu ya kifo.

“Naipongeza seŕikali ya Zimbabwe kwa kuungana na mataifa mengine 26 baŕani Afŕika ambayo yameondoa hukumu ya kifo,” alisema, pia akitambua maendeleo katika mataifa ya Ivory Coast, Ghana, Malaysia, Pakistan, na Zambia.

Turk aliashiria rekodi ya nchi 129 wanachama wa Umoja wa Mataifa kupiga kura kuunga mkono kusitishwa kwa hukumu ya kifo mnamo Disemba 2024 kama ushahidi wa kubadilika kwa mitazamo ya kimataifa.

Alitoa wito kwa nchi ambazo bado zinatumia adhabu ya kifo kuanzisha michakato ya kusitishwa kama hatua ya kwanza kuelekea kukomesha na kuhakikisha kuwa ni pale tu yanapotokea "makosa makubwa zaidi." Pia alizitaka mahakama kutumia busara kuzingatia hukumu mbadala, akisisitiza kuwa "hukumu ya kifo haisaidii kuwapa haki waathiriwa au kuzuia uhalifu."

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:AA
Soma zaidi
Trump ailalamikia Katiba ya Marekani kutomruhusu kuwania muhula wa tatu
Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita
Malkia wa zamani wa Thailand Sirikit afariki dunia akiwa na umri 93
Maseneta wa Marekani wanamtaka Trump kuchukua msimamo thabiti dhidi ya unyakuzi wa West Bank
Waziri Mkuu wa Israel amfuta kazi msaidizi wake mkuu wa usalama kwa mtafaruku juu ya Gaza
Mbu wapatikana nchini Iceland kwa mara ya kwanza
Kiongozi Mkuu wa Iran, Khamenei, apinga madai kuwa Marekani imeharibu uwezo wa nyuklia wa nchi yake
Mashambulizi mapya ya Israel yawauwa takriban Wapalestina 21 huko Gaza licha ya kusitishwa kwa vita
Gaza inaishutumu Israel kwa wizi wa viungo kutoka kwa Wapalestina, inataka uchunguzi wa kimataifa
ICC inakataa ombi la Israel la kukata rufaa kuhusu vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na Gallant
Israel yapunguza upatikanaji wa misaada kwa nusu, inazuia mafuta kuingia Gaza
Mabomu ambayo hayajalipuka yana hatari 'kubwa' huko Gaza, NGO yaonya
Marekani katika kizungumkuti cha kutumia dhahabu yake kulipia deni la taifa
'Sura mpya kwa amani' — Dunia inajibu baada ya kusaini hati rasmi ya kumaliza vita vya Gaza
Viongozi wa Marekani, Uturuki, Misri, na Qatar wamesaini makubaliano yanayositisha vita vya Gaza
Kuachiliwa kwa mateka kutaanza Gaza saa 11 alfajiri, vyombo vya habari vya Israel vinaripoti
Israel inadhulumu wafungwa Wapalestina kabla ya kuachiliwa chini ya makubaliano na Hamas, video inaonyesha
Trump, Sisi kushirikiana kuandaa mkutano wa Gaza huko Sharm el-Sheikh nchini Misri
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2025
Wapalestina 200,000 wanarejea kaskazini mwa Gaza huku wanajeshi wa Israel wakiondoka