| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mfalme Oyo mwenye umri mdogo zaidi duniani 34 afariki dunia
Mfalme Oyo wa Ufalme wa Tooro wa Uganda aliugua saratani, na alikuwa anatibiwa nchini Marekani, taarifa zilisema
Mfalme Oyo mwenye umri mdogo zaidi duniani 34 afariki dunia
Bendera ya Uganda.

Mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani,Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV, ambaye aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 3, amefariki dunia, Ufalme wa Tooro nchini Uganda ulitangaza siku ya Alhamisi. Alikuwa na umri wa miaka 34.

Alizaliwa Aprili 16, 1992, Oyo aliingia madarakani Septemba 12, 1995, kufuatia kifo cha baba yake, Mfalme Patrick David Matthew Kaboyo Olimi III.

Uongozi wa Kifalme unatambulika katika baadhi ya maeneo nchini Uganda, lakini ushawishi wao ni kwa jamii zaidi, kwa kuwa taifa linaongozwa na rais aliyechaguliwa.

Kutokana na umri wake mdogo, alisaidiwa na maafisa kadhaa ikiwemo mama yake, Malkia Best Kemigisa, na watendaji wengine wa Ufalme wa Tooro, na Rais wa Uganda Yoweri Museveni akimsaidia katika masuala ya ufalme hadi alipofika miaka 18.

Waziri Mkuu wa Ufalme wa Tooro Calvin Armstrong Rwomire Akiiki alitangaza kifo cha Oyo katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Marekani wa X.

“Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo cha Mheshimiwa Omukama (mfalme) wa Tooro, Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV, karibu saa nne usiku,” aliandika.

Hata hivyo, ufalme haukutoa taarifa zaidi kuhusu ugonjwa wa mfalme au hospitali aliyotibiwa na kufariki, lakini taarifa za vyombo vya habari zinadai kuwa alikuwa akiugua saratani na alikuwa anatibiwa Marekani.

“Hili ni pigo kubwa kwa Familia ya Kifalme, watu wa Tooro na taifa la Uganda. Taarifa rasmi itafuata na maelezo zaidi, ikiwemo kuhusu mipango ya mazishi na maombolezo,” kulingana na ufalme.

CHANZO:َAA