Utajiri wa Afrika: Shaba ya Afrika Magharibi
As Benin Bronzes return to Nigeria, the craft that made them struggles to survive / Reuters
Utajiri wa Afrika: Shaba ya Afrika Magharibi
Sanaa ya shaba imepoteza mvuto kwa sababu ya gharama kubwa ya uzalishaji, mbinu zinazohitaji nguvu kazi kubwa, hasa baada ya kuibuka kwa njia mbadala zenye gharama nafuu katika sanaa ya kisasa.

Afrika Magharibi, katika kipindi cha karne ya 16,  watu wa Benin na Ife na maeneo mengine katika eneo ambalo leo ni Nigeria walianza kutengeneza shaba kwa kutumia ustadi wa hali ya juu, ambapo baadhi yake bado ziko katika mfumo wa sanamu bora ulimwengu.

Sanaa ya shaba inajulikana pia na watu wengine wa Afrika Magharibi, kutoka Liberia hadi Cameroon.

Wataalamu katika Jiji la Benin la Nigeria walitengeneza mabango ya kina ya shaba, vitu vya ukumbusho, na vifaa kwa ajili ya mfalme wao  ili kuandika historia na heshima ya mababu zao.

Wasanii walitengeza kielelezo cha nta, kwa kawaida juu ya msingi wa udongo, wakaufunika kwa udongo, wakaupasha moto ili kuyeyusha nta, na kumwaga chuma kilichoyeyushwa ndani ya shimo katika kile kilichokuja kuitwa shaba ya Benin.

Kwa vizazi vingi, sanaa ya shaba ilikuwa ni kazi ya urithi inayohusishwa na ulezi wa kifalme na mila.

Kwa kawaida ilirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine.

Lakini, hivi sasa sanaa hii inaanza kutoweka kwa kasi baada ya kukosa mapato ya kuvutia kwa vijana.

Wataalamu wa shaba wanasema kizazi cha vijana wa sasa kinavutiwa zaidi na kipato kuliko uzuri wa kazi ya shaba, tofauti na mababu zao.

Sanaa ya shaba pia imepoteza mvuto kwa sababu ya gharama kubwa ya uzalishaji, mbinu zinazohitaji nguvu kazi kubwa, hasa baada ya kuibuka kwa njia mbadala zenye gharama nafuu katika sanaa ya kisasa.

Ingawa katika baadhi ya maeneo, bado mchakato huo kiasili wenye kutumia nta unaheshimiwa.

Wasanii chipukizi mara nyingi hawawezi kumudu gharama za nyenzo na ada za uanzilishi zinazohitajika kuunda, kufinyanga na kuunga vitu.

Sasa kuna taasisi chache maalum za shaba zinazopatikana, na hivyo kufanya iwe vigumu kwa wasanii kupata maeneo ya kufanyia kazi zao, jambo ambalo huongeza gharama na kuzuia ufikiaji.

Mtazamo wa sanaa ya kisasa umeelekezwa zaidi kwenye nyenzo mpya na teknolojia za kidijitali kama vile uchapishaji wa 3D.

Kwa hivyo wale waliothamini sanaa hii ya zamani wana wasiwasi kwamba ikiwa haitakuzwa kwa uzuri wake, itabaki katika vitabu vya kihistoria.

CHANZO:TRT Swahili