Uturuki na Ukraine zinadumisha ushirikiano wa kimkakati licha ya mapigano yanayoendelea, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan kufuatia kile alichokieleza kama ziara ya Kiev "iliiyokuwa na mafanikio makubwa" yaliyojikita katika ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, biashara na ulinzi wa kikanda.
Katika taarifa yake kupitia mtandao wa X siku ya Ijumaa, Fidan amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kina na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, Kiongozi wa Ofisi ya Rais Kyrylo Budanov na Waziri wa Mambo ya Nje Andrii Sybiha, wakiangalia yanayoendelea katika mapigano kati ya Urusi na Ukraine pamoja na njia za kuboresha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
"Tumeridhishwa kwamba ushirikiano kati ya nchi zetu mbili unaendelea kukuwa licha ya hali ya vita," Fidan amesema.
Amefurahishwa na Bunge la Ukraine kupitisha Makubaliano ya Biashara huru kati ya Uturuki na Ukraine kuelekea ziara yake, akielezea kuwa ni hatua muhimu ambayo itaongeza fursa mpya za biashara na vile vile kuboresha uhusiano wa kiuchumi kati yao.
Uturuki yasisitiza kuunga mkono amani
Katika ziara yake, Fidan amethibitisha uungaji mkono wa Uturuki kwa uhuru wa Ukraine, na hadhi ya mipaka, huku akisisitiza utayari wa Uturuki katika kuunga mkono jitihada za kuzileta upya Urusi na Ukraine katika meza ya mazungumzo.
"Uturuki iko tayari kuunga mkono kila jitihada ambazo zitarudisha pande zote mbili katika majadiliano na kuchangia amani ya kudumu," amesema.
Fidan pia amekutana na kiongozi wa kitaifa wa Crimea Tatar Mustafa Abdulcemil Kirimoglu na Mwenyekiti wa Crimean Tatar Mejlis Refat Chubarov kujadiliana hali ya jamii ya Crimea Tatar.
Amesema kulinda haki na kudumisha utambulisho wao itabaki kuwa kipaombele cha Uturuki.
Fidan pia ameshuruku baada ya kupokea nishati ya kiserikali kutoka kwa Rais Zelenskyy, na kusema ni fahari na kuishukuru serikali ya Ukraine.
Amesema, Uturuki itaendeleza urafiki wake wa muda mrefu na ushirikiano wa kimkakati na Ukraine katika misingi ya maono ya marais wa nchi hizo mbili iliyojikita katika uaminifu na maslahi ya pamoja.




















