Maelfu waandamana jijini Istanbul kuunga mkono Wapalestina
Wakiongozwa na viongozi wa dini na asasi za kiraia, maandamano ya “Hatuwezi Kunyamaza” yalikuwa na washiriki kutoka mashirika zaidi ya 400 yasiyokuwa ya kiserikali.
Maelfu wamekusanyika kote jijini Istanbul katika maandamano ya kuunga mkono Wapalestina, wakitoa wito wa kumalizwa kwa vita dhidi ya Wapalestina.
Maandamano hayo ya “Hatuwezi Kunyamaza, Hatuwezi Kusahau Palestina”, yaliyoandaliwa na Jukwaa la Muungano wa Mashirika yasiyokuwa kiserikali, lililoleta pamoja mashirika zaidi ya 400.
Washiriki walianza siku yao ya Alhamisi kwa kuswali swala ya Alfajiri katika miskiti mikubwa ikiwemo wa Ayasofya, Sultanahmet, Fatih, Suleymaniye, na Eminonu Yeni. Kutoka hapo, makundi mbalimbali yakaelekea kwenye daraja la Galata, wakiwa na bendera za Uturuki na Palestina, na kuvaa vilmeba vya keffiyeh, huku wakitamka maneno kama “Kutoka Istanbul hadi Gaza, maelfu ya salamu kwa mapambano” na “Palestina Huru.”
Bilal Erdogan, mwenyekiti wa Wakfu wa İlim Yayma, alihutumia umati huo, akisisitiza kuimarika kwa umoja wa raia. “Kila mwaka, watu zaidi wanashiriki, na leo tunaona uwezo wa umuhimu wa umoja wetu kama taifa,” alisema, akiongeza kwa dua ya uhuru wa wa Wapalestina na mji wa Jerusalem.
Viongozi wengine na wa mashirika ya kiraia na wa kidini, ikiwemo Abdullah Ozdemir, kiongozi wa chama cha AK tawi la Istanbul, na Rais wa Shirikisho la ONDER İmam Hatipliler Abdullah Ceylan, pia walijiunga nao.
Walioshiriki wlaibeba mabango yalikuwa na ujumbe “Haki kwa Wapalestina, Uadilifu kwa Dunia’’ na kila mara walipaza sauti zao kushtumu mashambulizi ya kikatili ya Israel. Waliojitolea waliwapa watu chai, supu, na kitafunwa cha simit.
Polisi waliimarisha ulinzi mkali katika njia yote iliyotumika kwa maandamano, lakini waandaaji waliyaeleza kuwa ya amani kuonesha umma unaunga mkono watu wa Palestina.
Washiriki wengi walieleza matumaini ya kuwa mwaka 2026 utakuwa wa haki, amani, na kumaliza mateso Gaza, wakiyataja maandamano “ujumbe mzito wa kuungana pamoja” kutoka Istanbul hadi Duniani.