| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Serikali ya Somalia yasikitishwa na hatua ya kuzuiwa kwa mwamuzi wa nchi hio kuingia Marekani
Serikali ya Somalia ilifanya juhudi za kidiplomasia na mamlaka husika, lakini hazikuzaa matokeo chanya, wizara ya mambo ya nje yasema.
Serikali ya Somalia yasikitishwa na hatua ya kuzuiwa kwa mwamuzi wa nchi hio kuingia Marekani
“Tunasikitishwa, juhudi hizi hazikuleta matokeo yaliyotarajiwa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilisema katika taarifa. / / AA

Serikali ya Somalia Jumatano ilieleza masikitiko yake kuhusu uamuzi wa kunyimwa kuingia Marekani kwa mwamuzi wa kimataifa wa Somalia, Omar Abdulkadir Artan, ambaye alitarajiwa kuchezesha mechi za Kombe la Dunia 2026.

Kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje, nchi hiyo imetoa taarifa rasmi kwa mara ya kwanza kuhusu suala hilo. Kulingana na taarifa hio serikali ya Somalia ilisema kwamba ilifanya juhudi za kidiplomasia na mamlaka husika ili kusaidia safari ya Artan.

“Tunasikitika, juhudi hizi hazikuleta matokeo yaliyotarajiwa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia ilisema katika taarifa.

“Somalia itaendelea kushirikiana na wadau husika kutafuta ufafanuzi zaidi kuhusu suala hili na kulinda hadhi pamoja na haki za raia wake,” taarifa hiyo iliongeza.

Artan aliwasili katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, akitokea Uturuki mapema Jumatano, ambapo alipokelewa kwa shangwe kubwa.

CHANZO:TRT Afrika