China imepinga vitisho vya kijeshi vya Marekani, inavyovifanya dhidi ya kisiwa hicho.
Kulingana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian, Marekani ilikuwa ikiratibu operesheni mbalimbali za kijeshi, ikiwemo kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya Cuba.
"Tumepata taarifa hizo. Matumizi ya vitisho vya aina hiyo, ni ukiukwaji mkubwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na unahatarisha usalama na amani ya kikanda," alisema Lin, akiongeza kuwa China inapinga hatua hiyo.
ZILIZOPENDEKEZWA
Waziri huyo, aliongeza kuwa China itaendelea kuiunga mkono Cuba, katika kulinda utawala wake na kutokuingiliwa na mataifa ya nje.
CHANZO:Anadolu Agency


















