tokea masaa 3
Bilionea Bill Gates anatarajiwa kusimama mbele ya kamati ya bunge la Marekani kutoa ushahidi wake kuhusu tuhuma za biashara haramu ikiwemo usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, zinazomkabili Jeffrey Epstein.
Muasisi huyo wa kampuni ya Microsoft, ni kati ya majina makubwa yaliyohusishwa na Epstein.
Kulingana na vyanzo vya karibu na Gates, bilionea huyo atahojiwa na kamati hiyo, kama ilivyokuwa kwa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, na mkewe Hillary.
Gates amewahi kukiri kutenda kosa kubwa, kwa kujihusisha na Epstein, akisema uhusiano huo uliathiri kazi za taasisi zake.
CHANZO:AFP














