Baraza la Mawaziri la Zimbabwe lamuongezea muda wa kukaa madarakani Rais Emmerson Mnangagwa
Mabadiliko hayo yanakuja miezi mitano baada ya chama cha Zanu-PF, kupitisha maazimio ya kumuweka madarakani kiongozi huyo mwenye miaka 83 madarakani, hadi 2030.
Baraza la Mawaziri la Zimbabwe limepitisha mabadiliko kwenye katiba ya nchi hiyo, ambayo yanalenga kumuongezea Rais Emmerson Mnangagwa, muda zaidi wa kukaa wa madarakani.
Mawaziri hao wamependekeza Mnangagwa aendelee kuwa madarakani kwa miaka miwili zaidi, mpaka mwaka 2030.
Mabadiliko hayo yanakuja miezi mitano baada ya chama cha Zanu-PF, kupitisha maazimio ya kumuweka madarakani kiongozi huyo mwenye miaka 83 madarakani, hadi 2030.
Kulingana na Waziri wa Sheria wa Zimbabwe Ziyambi Ziyambi, muswada huo utapelekwa kwanza spika wa bunge la nchi hiyo, na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kabla haujapitishwa na wabunge.
Mnangagwa aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, akimuondoa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe mwaka 2017.
Hata hivyo, vyama vya upinzani vimepinga michakato ya chama cha Zanu-PF cha kumuongezea Mnangagwa muda wa kukaa madarakani.