Ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Israeli Isaac Herzog imesafiri kwa muda wa saa nane kwenda Kazakhstan kwa ziara yake ya siku mbili. Ndege hiyo ililazimika kufuata njia mbadala ambayo ni ndefu zaidi kwa kupitia Ulaya na Urusi ili kuepuka kuingia katika anga ya Uturuki.
Kituo cha televisheni cha Israel, Channel 12 kiliripoti kwamba ndege hiyo ilifuata njia mbadala kupitia Ulaya na Urusi ili kuepuka kuingia katika anga la Uturuki, na kuongeza muda wa safari hiyo kuwa ya saa nane.
Kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii X, Herzog alithibitisha kuwa amewasili katika mji wa Astana.
Mnamo Novemba 2024, Uturuki pia ilimnyima Herzog ruhusa ya kutumia anga yake kwenda katika mkutano wa COP29 uliofanyika Baku, ambapo baadaye alighairi safari hiyo akitaja sababu za “hofu ya usalama.”
Mahusiano kati ya Uturuki na Israel yameendelea kuzorota tangu vita vya Israel dhidi ya Gaza, ambavyo baadaye vilipanuka na kuhusisha pia Lebanon na Iran.













