Vita vya Daudi na Goliati kati ya Wasomali na Donald Trump
Cheche za matusi katika majukwaa hazitotoa muelekeo wa mustakabali, bali ni katika uwezo, umoja, na uthabiti wa msimamo wa jamii inayolaumiwa.
Na Mohamed Guleid
Rais Donald Trump amekuwa na misimamo mikali. Mbabe, kupenda ugomvi ndiko kunakotoa taswira ya maisha yake ya siasa na kuratibu mijadala duniani kwa zaidi ya muongo mmoja.
Wengine wanapenda aina yake ya siasa, wengine wanaona hana busara, lakini wakati wa kampeni za uchaguzi wa Urais 2024, hata wale ambao wanatofautiana naye wakati mwingine wanakubali kuwa misimamo yake ni ya kutoka moyoni katika mazingira ya sisasa ambapo hotuba zinakuwa rasmi sana.
Tangu kurejea kwake Ikulu kwa mara ya pili, kauli za Trump zimezidi kuwa kali na kuzua maswali kuhusu uelewa wake wa mifumo ya Marekani.
Kauli zake za hivi karibuni dhidi ya jamii ya Wasomali — kuita jamii nzima watu “wasiokuwa na maana” zilishangaza wengi. Haikuwa tu kauli ambayo ililenga kutawala vichwa vya habari.
Ilikuwa ni matusi yaliyolenga watu ambao wanaishi katika nchi hiyo kisheria, wengi wao wakiwa katika nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30.
Haya hayakuwa makabiliano ya kwanza ya Trump na jamii ya Wasomali nchini Marekani. Mwakilishi Ilhan Omar, rais wa Marekani mwenye asili ya Somalia kutoka Minnesota, amekuwa mmoja ya wale wanaolengwa.
Mkakati wa kisiasa?
Kwa miaka kadhaa, Trump amekuwa akitumia lugha mbaya na wakati mwingine ya kejeli dhidi yake, mara nyingi akikiuka maadili hata kwa wanachama wa chama chake mwenyewe. Mtindo huu unazua swali la msingi: ni Trump kuonesha uhalisia, au kuna mkakati mkubwa zaidi kwa mvutano huu?
Matokeo mabaya
Hata hivyo, historia, inatuonya kuhusu matokeo ya mtindo kama huo. Wakati viongozi wenye uwezo wanapolenga jamii ya walio wachache kwa nia ya kisiasa, matokea yanaweza kuwa mabaya sana.
Kama ilivyokuwa katika historia ya Uhispania katika karne ya 15, kipindi Wayahudi na Waislamu walivyonyanyapaliwa, kushtumiwa kwa kuwa kutokuwa watiifu, na baadaye wakafukuzwa au kulazimishwa kuingia dini nyingine bila hiari yao.
Mchakato huo haukuanza na vurugu; ulianza kwa watu kwua na hofu, lugha ya matusi, na viongozi kuona jamii nzima kama tishio. Matamshi yaliyoweka msingi wa ubaguzi.
Wakati Marekani ina ulinzi wa kikatiba, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, na kinga kwa taasisi, matamshi kutoka kwa rais aliye madarakani yana ushawishi mkubwa.
Uhamiaji, ufuatiliaji, na sera ya ujumuishaji kunaweza kuwaathiri Wasomali na Waislamu wengine. Na matokeo yake yanaweza kuenea hadi Afrika Mashariki, kuathiri maisha ya familia, kutuma fedha, uhusiano na raia wa nje, na ushirikiano wa kidiplomasia.
Mwishowe, mvutano wa kweli kati ya Trump na Wamarekani wenye asili ya Somalia. Ni kati ya dira mbili katika jamii -moja ambayo inaona watu kuwa pamoja kama uwezo na nyingine ambayo inaona tofauti za watu kama jambo la kutia hofu.
Raia wa Marekani wenye asili ya Somalia wana fursa ya kujibu mashambulio haya kwa kuonesha ustahmilivu, kujihusisha kama majukumu ya kiraia, kuungana pamoja, na kudhihirisha nafasi yao katika taifa la Marekani.
Matamshi ya Trump yanaweza kuwa yanalenga kuwadunisha, lakini historia inaonesha jamii iliyo na heshima na kujihusisha katika masuala ya demokrasia huwa inaishi zaidi ya viongozi kuwepo madarakani ambao wanategemea kugawanya watu.
Matusi yanayotolewa kwenye majukwaa hayatobaini mustakabali wa nchi, bali ni katika uwezo, umoja, na uthabiti wa jamii inayolaumiwa.
Mwandishi, Mohamed Guleid ni Naibu Gavana wa zamani wa Kaunti ya Isiolo, Kenya.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, muelekeo na sera za uhariri za TRT Afrika.