| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Idadi ya watumishi wa afya waliofariki Ziwa Tanganyika nchini Tanzania yafikia saba
Wafanyakazi wa afya walikuwa wakisafiri kwenda kijiji cha karibu na mpaka wa Burundi wakati mashua yao ilipopinduka na kuzama.
Idadi ya watumishi wa afya waliofariki Ziwa Tanganyika nchini Tanzania yafikia saba
Wengine 14 wameokolewa na wanaendelea kupatiwa matibabu. Picha/JMakamba / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 3

Takriban watumishi saba wa afya wamefariki nchini Tanzania baada ya boti yao kukumbwa na dhoruba kati katika Ziwa Tanganyika siku ya Ijumaa, imethibitisha Ofisi ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kundi hilo la watumishi wa afya lilikuwa linakwenda kutoa huduma ya afya katika kijiji cha Kagunga kilichopo katika mpaka wa Tanzania na Burundi pindi boti yao ilipopinduka na kuzama, imeongeza kusema taarifa kutoka Ofisi ya Rais.

Wengine 14 wameokolewa na wanaendelea kupatiwa matibabu, huku vikosi vya uokoaji vikiendelea kuwatafuta wengine wawili.

Eneo hilo lina maelfu ya wakimbizi kutoka Burundi, ambao hivi karibuni wameanza kurudi nchini mwao baada ya miaka mingi ya kuwa Tanzania, hii ni baada ya mamlaka kuamua kufunga kambi zao.

Watumishi wa afya na mashirika ya kutoa misaada yamekuwa yakitoa huduma kwa wakimbizi.

Katika tukio jengine katika Ziwa Tanganyika, mvuvi mmoja alifariki na wengine kujeruhiwa baada ya boti yao kupigwa na radi, taarifa hiyo iliongeza.

Rais Samia alitoa salamu zake za rambi rambi kufuatia msiba huo.

Eneo la Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni limeshuhudia dhoruba kali ya upepo, huku takriban 80 wakipoteza maisha katika mafuriko na maporomoko kusini mwa Ethiopia, na zaidi ya watu 60 wakifariki nchini Kenya.