Chama cha wafanyakazi wa Migodi cha Ghana kimewasilisha malalamiko benki kuu siku ya Alhamisi kikitaka zaidi ya cedi milioni 380 ($34.55 milioni), wanazosema ni zao na kudai kuwa zimezuiwa tangu waanze ufuatiliaji wa sekta ya fedha.
Kulingana na mabadiliko yalioanza Agosti 2017 na kukamilika kuangazia misingi ya usimamizi dhaifu wa fedha, benki kuu ilifuta leseni za taasisi za fedha zaidi ya 400.
Chama cha Wafanyakazi wa Wachimba Migodi cha Ghana, ambacho ni sehemu ya Chama Kikuu cha Wafanyakazi, kinasema pesa zilizoko kwenye mfuko wa akiba na za kiinua mgongo ni za wafanyakazi zaidi ya 19,000 na bado zimezuiwa kutokana na hali hiyo.
Wizara ya fedha haijazungumzia chochote kuhusu hayo.
Katibu Mkuu Abdul-Moomin Gbana anasema miongoni mwa wanachama wanaokabiliwa na tatizo hili ni wastaafu, walioachishwa kazi, wajane na wanaowategemea ambao wanapata tabu kupata matibabu, elimu na kukimu gharama za maisha.
Chama hicho kinasema kimewasihi wanachama kutofanya maandamano tangu 2021, kutokana na hakikisho la benki kuu.
Chama kimetishia kufanya maandamano na kutaka kukutana na gavana wa Benki Kuu ya Ghana pamoja na waziri wa fedha.













