| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Rais wa China asema hatoipatia Iran silaha: Trump
“Alisema hatatoa vifaa vya kijeshi. Hio ni kauli muhimu sana", Rais Trump wa Marekani amesema baada ya kukutana na Rais Xi wa China, akiongeza kuwa China inataka kuona Mlango-Bahari wa Hormuz ukifunguliwa.
Rais wa China asema hatoipatia Iran silaha: Trump
Rais wa Marekani Trump amesema China inataka Mlango wa Hormuz uwe wazi. / / Reuters

Rais wa Marekani Donald Trump amedai kwamba Rais wa China Xi Jinping alimwambia kuwa China haitoipatia Iran vifaa vya kijeshi, na pia anaunga mkono kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

Trump alisema hayo baada ya kukutana na Xi mjini Beijing, katika mahojiano na shirika la habari la FOX News.

“Alisema hatatoa vifaa vya kijeshi. Hio ni kauli muhimu sana", Trump alisema alipoulizwa kama walizungumzia kuhusu msaada wa China kwa Iran.

Trump pia aliongeza kuwa Xi alisema China inataka Mlango-Bahari wa Hormuz ubaki wazi, kwa sababu China hununua kiasi kikubwa cha mafuta kutoka eneo hilo.

“Alisema wananunua mafuta mengi huko, na wanataka kuendelea kufanya hivyo,” Trump alisema.

Aliongeza pia kuwa Xi angependa kuona makubaliano yakifikiwa kuhusu suala hilo, na alisema yuko tayari kusaidia inapowezekana.

Hata hivyo, mamlaka za China hazikutoa ufafanuzi wowote hadi sasa kuhusu madai ya Trump.

Taarifa rasmi ya China kuhusu mazungumzo hayo haikuzungumzia Iran wala Mlango-Bahari wa Hormuz. Ilisema tu kuwa viongozi hao wawili walijadili masuala muhimu ya kimataifa na kikanda, ikiwemo hali ya Mashariki ya Kati, mgogoro wa Ukraine, na rasi ya Korea.

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Iran yasema makombora yako tayari huku vitisho vya Israel dhidi ya Beirut vikiongezeka
Raia wa Australia akamatwa kwa kufuga mende zaidi ya laki moja
Kiongozi wa upinzani Guinea Bissau awekwa kifungo cha nyumbani
Waafrika waliokuwa India kwa matibabu, miongoni mwa 21 waliofariki katika ajali ya moto hotelini
Iran yashambulia uwanja wa ndege wa Kuwait
Iran yashambulia kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Kuwait, 7 wajeruhiwa
Uingereza kuzindua chombo cha AI kugundua wahamiaji watu wazima wanaodai kuwa watoto
Serikali ya Trump inataka noti ya $250 inayoonesha picha yake: ripoti inasema
Syria yagundua mkusanyiko wa silaha za kemikali kutoka mpango wa zamani wa serikali ya Assad
Tumeshambulia kambi ya jeshi la Marekani nchini Kuwait: Vikosi vya Iran (IRGC)
Waislamu waswali swala ya Eid al-Adha katika Msikiti wa Al-Aqsa
Takriban Waislamu milioni 2 wanatarajiwa kutekeleza ibada ya Hajj huku mahujaji wakielekea Mina
Israel inahofia kuwa Trump atafuata makubaliano yenye mipaka ya Iran, na kuacha mpango wa nyuklia
'Wamepata vidonda mwilini' — wanaharakati wasimulia mateso waliyopitia walipotekwa na Israel
Mojtaba Khamenei amesema madini ya urani ya Iran yatabaki nchini humo
Marco Rubio: Tutahakikisha Ebola haifiki Marekani
Wanaharakati wa msafara wa Flotilla walioshambuliwa na Israel wapelekwa Uturuki
Trump na Netanyahu watofautiana kwa njia ya simu kuhusu kuishambulia Iran — Ripoti
Marekani na Israel zilipanga kumuweka madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo Ahmadinejad
Urusi na China zaimarisha ushirikiano kwa kusaini mikataba 20 ikiwemo ya uchumi, nishati na biashara