tokea masaa 10
Makombora na droni kutoka Urusi yameua watu 16 na kujeruhi zaidi ya 80 nchini Ukraine, katika kipindi cha wiki mbili, serikali ya Ukraine imethibitha.
Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha, Urusi ilituma makombora 700 na kulenga raia wa kawaida.
ZILIZOPENDEKEZWA
Watu wapatao wanne waliuawa mjini Kyiv, akiwemo mtoto wa miaka 12, huku wengine zaidi ya 50 wakijeruhiwa.
“Matukio ya namna hii yasichukuliwe kuwa ya kawaida, ni lazima yasitishwe na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Sybiha.









