MICHEZO
1 dk kusoma
Namibia na Zimbabwe zafuzu kwa Kombe la Dunia la Kriketi T20 mwaka 2026
Zimbabwe imeungana na Namibia katika kufuzu Kombe la Dunia T20 kwa wanaume baada ya kuifunga Kenya kwenye nusu fainali ya pili kwa Afrika mjini Harare. Nchi ya tatu kufuzu ni Afrika Kusini, ambao walipata tiketi ya moja kwa moja kwa Kombe la Dunia.
Namibia na Zimbabwe zafuzu kwa Kombe la Dunia la Kriketi T20 mwaka 2026
Timu ya Kriketi ya Namibia. / Reuters
3 Oktoba 2025

Namibia na Zimbabwe wamejihakikishia nafasi zao kwenye Kombe la Dunia la Kriketi T20 mwaka 2026 baada kutinga fainali za kanda ya Afrika mjini Harare siku ya Alhamisi.

Timu zote mbili zimefuzu kwa mashindano ambayo yatakuwa na wenyeji wenza India na Sri Lanka kati ya mwezi Februari na Machi mwakani.

Namibia iliifunga Tanzania kwa mikimbio 63 katika nusu fainali iliyokuwa na msisimko mkubwa. Zimbabwe nayo ikaigaragaza Kenya katika uwanja wa nyumbani Harare na kuwa timu ya 17 kufuzu kwa Kombe la Dunia T20 mwaka 2026.

Namibia na Zimbabwe watapambana kwenye fainali ya Kanda ya Afrika Oktoba 4, lakini timu zote mbili zimefuzu kwa mashindano ya Kombe la Dunia.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Ligi Kuu ya England (EPL) kurindima tena baada ya mapumziko
Nini Nigeria ifanye kufuzu Kombe la Dunia 2026?
Ndege ya timu ya soka ya Nigeria iliyokuwa inaelekea nyumbani yalazimika kutua kwa dharura
Algeria yafuzu kwa Kombe la Dunia 2026
Timu ya raga ya Afrika Kusini mabingwa wa dunia tena
Kenya yashinda afueni ya vikwazo vya matumizi ya dawa za kusisimua misuli
Arsenal na Newcastle wapata ushindi kwenye mechi za Ligi ya mabingwa barani Ulaya
India yagoma kushiriki hafla ya kombe baada ya kuipiga Pakistan kutwaa taji la Kombe la Asia
Wanariadha wa Kenya Wanakaribishwa Kwa Shangwe Baada ya Ushindi Wao Katika Tokyo
Nyota wa Ufaransa na PSG Ousmane Dembele Ashinda Ballon d'Or 2025
Botswana yaweka historia kwa kushinda dhahabu ya kusisimua ya 4x400m
Lilian Odira wa Kenya ameshinda dhahabu ya dunia katika mbio za 800m kwa kumshinda Hodgkinson
Wakenya washinda mbio za marathon za wanaume na wanawake mjini Berlin
Mkenya Peres Jepchirchir ampiku Tigst Assefa wa Ethiopia kupata dhahabu katika mbio za marathon
Alphonse Simbu adakia dhahabu ya kwanza kabisa kwa Tanzania Katika Mashindano ya Dunia ya mbio-Tokyo
Omar Artan aweka historia ya kuwa mwamuzi wa kwanza wa Somalia kuchezesha Kombe la Dunia la FIFA
Morocco iliishinda Niger na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026
Kipa Mbrazil Ederson ajiunga na Fenerbahce ya Uturuki akitokea Manchester City
Morocco yaipiga Madagascar na kushinda taji la tatu la CHAN
Abdou Abdel Mefire ameteuliwa kuwa mwamuzi katika fainali ya CHAN PAMOJA 2024 jijini Nairobi