Afcon 2025: Andre Onana hayuko kwenye kikosi cha Cameroon, kocha atimuliwa
Andre Onana, ambaye yuko katika timu ya Trabzonspor kwa mkopo kutoka Manchester United, hakutajwa miongoni mwa makipa wanne katika kikosi cha wachezaji 28.
Kocha Mbelgiji wa Cameroon Marc Brys siku ya Jumatatu alifutwa kazi, na golikipa wa Manchester United Andre Onana hakujumuishwa kwenye kikosi cha Afcon 2025 inayotarajiwa kuanza Disemba 21 nchini Morocco.
Brys amekuwa na uhusiano mbaya na rais wa shirikisho la soka la taifa hilo na mchezaji nyota wa zamani Samuel Eto'o kwa hiyo kutimuliwa kwake siyo jambo la ajabu baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026.
Cameroon, ambayo imecheza katika ngazi ya Kombe la Dunia mara nane na ni rekodi kwa bara la Afrika, ilifungwa na timu ambayo haikupewa nafasi ya Cabo Verde ili kupata nafasi ya moja kwa moja kuelekea kwenye michuano hiyo itakayofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Wakapata fursa ya pili kama moja ya timu nne bora zilizomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi, Cameroon ikafungwa 1-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nchini Morocco mwezi uliopita na kuondolewa.
Kocha mzawa
Eto'o alichaguliwa tena rais wa shirikisho la soka la nchi FECAFOOT kwa muhula wa pili mwishoni mwa wiki, na moja ya maamuzi yake ya kwanza ni kumfuta kazi Brys na kumteua kocha mzawa David Pagou.
Pagou mwenye umri wa miaka 56 amewahi kufunza vilabu kadhaa nchini Cameroon, ikiwemo Coton Sport, timu ambayo imekuwa ikifanya vizuri zaidi katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.
Andre Onana, ambaye yuko katika timu ya Trabzonspor kwa mkopo kutoka Manchester United, hakutajwa miongoni mwa makipa wanne katika kikosi cha wachezaji 28.