Kutoka Baghdad hadi Abuja: Muenendo wa Marekani wa zamani wa uhuru na uharibifu

Madai ya Trump kuhusu mauaji ya halaiki ya Wakristo nchini Nigeria na vitisho vya mashambulizi ya kijeshi ni muenendo waliyozowea Marekani kwa kisingizio cha misaada kwa watu.

By
Trump atishia Marekani itashambulia Nigeria kutokana na wanayowatendea Wakristo

Na Abu Bilaal Abdulrazaq bn Bello bn Oare

“Nyoka anayejitolea kukuimbia anafanya hivyo kukupima anaweza kukugonga vipi kwa ukaribu.” 

Huu ni msemo wa zamani wa Kiafrika ambao unaonya kuhusu kuamini watu bila kutafakari — kwa watu ambao wanaamini kila kitu kinachosemwa na mataifa ya nje, wanaweza kupoteza busara yao na uhuru. 

Kwa bahati mbaya, hii ndiyo njia inayoonekana kufuatwa na Nigeria baada ya tamko la hivi karibuni la Rais wa Marekani Donald Trump, kuieleza Nigeria kama nchi ambayo wana jambo nayo na kudai, bila kutoa ushahidi wowote, kwamba Wakristo nchini Nigeria wanakabiliwa na mauaji ya halaiki. 

Trump alionya kuwa kama serikali ya Nigeria “itaendelea kuruhusu kuuawa kwa Wakristo, Marekani itasitisha misaada kwa Nigeria mara moja, na inaweza kuvamia nchi hiyo ambayo inatia aibu kwa sasa, ’ ili kuangamiza kabisa magaidi wa Kiislamu ambao wanatekeleza ukatili mbaya sana”. 

Matamshi yake yamezidisha kutoaminiana miongoni mwa jamii mbalimbali, ambazo kwa miaka mingi,imekuwa ikijitahidi kuponya vidonda vya tofauti za kidini. 

Kutoka Iraq hadi Libya, Afghanistan hadi Somalia, uvamizi wa Marekani umesababisha uharibifu kwa mataifa — kutatiza, kugawanya, na kuyaacha yakiwa katika hali mbaya kuliko yalivyokuwa. 

Yote haya kwa kisingizio cha kuleta demokrasia, uhuru, au wasiwasi kuhusu hali za watu. Lakini pale mambo yanapotulia, ule unaosemekana kuwa uhuru unasababisha vurugu, na ukosefu usalama wa muda mrefu.

Kufikiria kwamba itakuwa tofauti kwa Nigeria kwa “wasiwasi huo” ni kubeza matukio ya kihistoria. 

Hatari zaidi, huenda ikasababisha raia wa Nigeria kukabiliana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya kidini, raia dhidi ya raia, wakati ambapo umoja na maelewano yanahitajika zaidi nchini humo.

Unafiki huu unakuwa mkubwa wakati mtu anapoangalia nje ya mipaka ya Nigeria. 

Kufikia Novemba 3, 2025, watu zaidi ya 68,858 wameuawa na wengine zaidi 170,664 kujeruhiwa Gaza, kulingana na Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza, kwenye idadi ya watu karibu milioni 2.2. 

Na bado Trump hajatangaza Gaza “kuwa nchi ambayo wana jambo nayo”. 

Hajatoa wito wa kusaidia huko. Kwa nini? Kwa sababu wengi ya wanaouawa ni Waislamu. Undumakuwili huu ni wa wazi.

Ukiangazia kwa makini, kwa muda mrefu Marekani yenyewe imekuwa ikiendeleza vita dhidi ya mataifa ya Kiislamu kwa visingizio vingi — kukabiliana na ugaidi, kulinda amani, kuwapelekea watu misaada. 

Nigeria isiwe sehemu nyingine ya mchezo wao. 

Nigeria ni nchi huru. Mara kadhaa serikali yake imekanusha kuhusika na madai ya mauaji ya halaiki dhidi ya Wakristo. 

Hakuna kiongozi wa kigeni, hata awe na uwezo au na fujo vipi, ambaye ana haki nchini ya sheria ya kimataifa kuanzisha operesheni za kijeshi katika mipaka yetu. 

Kufanya hivyo itakuwa ni uchokozi, hakuna mjadala. 

Katika nyakati hizi, Wanigeria lazima wafikirie kwa makini, siyo kwa mihemko. Hatari yenyewe siyo maneno ya Trump — bali sisi wenyewe kukubali matamshi yake. 

Kama watu wenye hekima wanavyosema, “Wakati mtu wa nje anakwambia mchuzi wa mama yako una ladha nzuri kuliko wa kwako, anataka tu umpe kijiko chako.”