| swahili
UTURUKI
3 dk kusoma
Uturuki yatuma msaada wa kibinadamu Afghanistan kufuatia tetemeko la ardhi
Mkoa wa Kunar pekee uliripoti vifo 1,411, huku 3,124 wamejeruhiwa, na nyumba 5,412 ziliharibiwa.
Uturuki yatuma msaada wa kibinadamu Afghanistan kufuatia tetemeko la ardhi
Mkoa wa Kunar ndio mkoa ulioathiriwa zaidi mashariki mwa Afghanistan, ambapo zaidi ya watu 1,400 wamekufa hadi sasa. /
3 Septemba 2025

Uturuki imetuma msaada wa kusaidia watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi katika jimbo la Kunar nchini Afghanistan huku shughuli za uokoaji zikiingia siku ya tatu.

Tetemeko hilo kubwa lilisababisha maelfu ya watu kukosa makazi na vijiji kuwa magofu.

"Katika kukabiliana na maafa ya tetemeko la ardhi katika jimbo la Kunar la Afghanistan, ndege ya A400M ya Jeshi letu la Anga imeondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kayseri/Erkilet kupeleka misaada kwa watu iliyotayarishwa na AFAD na Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki," Wizara ya Ulinzi ya Uturuki ilitangaza siku ya Jumatano kupitia mtandao wa X.

Afisa wa Taliban katika jimbo la Kunar, akizungumza na Anadolu kwa sharti la kutotajwa jina, alisema baadhi ya vifaa vya msaada vilianza kuwasili jana usiku katika baadhi ya maeneo ya mbali ambako uongozi wa mpito ulipopanga awali kuwahamisha watu katika maeneo salama.

"Wenyeji walikataa kuondoka kwa sababu miili ya wapendwa wao bado ilikuwa chini ya vifusi. Kisha tukaanza kusambaza mahema na vitu vingine muhimu," afisa huyo alisema.

Mkoa wa Kunar ndio eneo lililoathiriwa zaidi mashariki mwa Afghanistan, ambapo zaidi ya watu 1,400 wamekufa hadi sasa. Maafisa walisema eneo la milimani na barabara zilizoharibika zimefanya kuwa vigumu kutoa msaada, lakini maafisa wa uokoaji na misaada bado wamefika katika maeneo yote yaliyoathiriwa.

"Tunapelela misaada kwa magari inapowezekana, lakini katika maeneo yaliyokatizwa na tetemeko la ardhi, helikopta zinatumiwa kusafirisha vifaa na kuwahamisha waliojeruhiwa hospitalini," afisa huyo alisema.

'Changamoto kubwa'

Abdul Wahid, mkazi wa eneo la mkoa wa Kunar, alisema athari za mitetemeko bado zinaendelea, na kueneza hofu miongoni mwa umma.

Siku ya Jumanne, tetemeko jipya la ardhi la kipimo cha 5.2 lilipiga kaskazini mashariki mwa Afghanistan ambayo pia ilisikika kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Mashirika ya misaada yanaonya kwamba kiwango cha uharibifu kinahitaji msaada wa haraka wa kimataifa ili kuzuia mzozo unaozidi kuwa mbaya.

Siku ya Jumanne, Mratibu wa Misaada kwa Watu Umoja wa Mataifa kwa Afghanistan, Indrika Ratwatte, alisema kuwa tetemeko hilo la ardhi lilipiga mashariki mwa Afghanistan wakati wa machafuko mengi yanaendelea katika nchi hiyo.

"Kwa hivyo, ukiangalia takwimu, ukiangalia umbali na hali ya juu ya ardhi, ambayo ni changamoto kubwa pamoja na kuwa ni mbali, kuna uwezekano wa watu walioathiriwa kufikia karibu mamia ya maelfu," Ratwatte alisema.

Idadi ya vifo inaweza kuongezeka

Mataifa kadhaa zaidi, ikiwa pamoja na nchi jirani za Pakistan, Iran, China, na India, pamoja na mataifa ya Magharibi, yameahidi kupeleka misaada Afghanistan.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya mpito Zabihullah Mujahid, jimbo lililoathiriwa zaidi la Kunar pekee liliripoti vifo 1,411, na wengine 3,124 kujeruhiwa, wakati nyumba 5,412 ziliharibiwa.

Idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi wakati mamlaka itashiriki data kutoka majimbo mengine matatu ya Nangarhar, Laghman, na Panjshir.

Uchunguzi wa Jiolojia wa Marekani ulirekodi tetemeko hilo saa 11.47 jioni kwa saa za huko (1917 GMT), lililoko kilomita 27 (maili 16.7) mashariki-kaskazini-mashariki mwa Jalalabad katika kina cha kilomita 8 (maili 5) Jumapili usiku, wakati wakazi wengi walikuwa wamelala.

Hili ni tetemeko kubwa la tatu la ardhi kuwahi kukumba taifa lililokumbwa na vita tangu kurudi kwa kundi la Taliban la Afghanistan mamlakani mnamo Agosti 2021.

CHANZO:TRT World and Agencies
Soma zaidi
Uturuki inamkumbuka Ataturk miaka 87 baada ya kufariki
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki kuzuru Marekani siku ya Jumatatu
Rais Erdogan anatumai Marekani itatimiza ahadi zake kuhusu makubaliano ya ndege za kivita za F-35
Palestina inapongeza amri za kukamatwa dhidi ya maafisa 37 wa Israel kutoka Uturuki kama 'ushindi
Ujumbe wa Erdogan 'Azerbaijan haiko peke yake' ulipelekea ushindi wa Karabakh: Aliyev
Ushindi wa Karabakh wa Azerbaijan kwa amani ya Caucasus: Rais Erdogan
Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu, juu ya mashtaka ya mauaji
Erdogan: Uturuki kuharakisha miradi ya kiulinzi kuimarisha ‘maslahi’ na washirika wa Ulaya
Uturuki kuandaa mazungumzo ya Gaza wiki ijayo kufuatia wasiwasi juu ya usitishaji mapigano – Fidan
Mfumo wa ulimwengu wa sasa unazingatia nguvu zaidi ya haki: Mkurugenzi wa TRT
Israel imeigeuza Gaza kuwa vifusi, inawezaji kuwa haina hatia: Erdogan
Uturuki yakashifu unafiki wa nchi za Magharibi kuhusu Gaza, yatoa wito wa mfumo mpya wa dunia
Hamas haina nuyklia, Israel iko nayo: Erdogan aitaka Berlin ichukue hatua kali dhidi ya Tel Aviv
Erdogan ataka kuona mabadiliko katika uhusiano na EU na ushirikiano wa kikanda alipokutana na Mertz
Ujerumani yatoa wito wa kuunda “ushirikiano wa kimkakati” ili kukabiliana na changamoto za kimataifa
"Marekebisho ya Ulimwengu": Jukwaa la 9 la TRT World kuanza Istanbul likiangazia majadiliano na haki
Erdogan ametangaza washindi wa Tuzo Kuu za Utamaduni na Sanaa za Urais mwaka 2025
Uturuki yaadhimisha miaka 102 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri
Uturuki yatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mji wa Al Fasher, Sudan
Uturuki na Jordan zasaini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi