| Swahili
AFRIKA
3 dk kusoma
Kutoka kwa Kaunda hadi Hichilema: Marais wa Zambia tangu uhuru
Zambia imekuwa na marais saba na kaimu rais mmoja, huku ikionekana kama moja ya nchi za Kusini mwa Afrika yenye ukomavu wa demokrasia.
Kutoka kwa Kaunda hadi Hichilema: Marais wa Zambia tangu uhuru
Zambia imekuwa na marais saba na kaimu rais mmoja tangu nchi hiyo kupata uhuru.

Zambia inajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu Agosti 13, huku Rais Hakainde Hichilema akiwania muhula wa pili na viti 226 vya ubunge kuwaniwa.

Lakini unajua ni kina nani wameongoza Zambia tangu kupata uhuru 1964?

Hii ndio safari ya kisiasa ya nchi hiyo.

Imejizolea sifa ya kuwa moja ya nchi za Kusini mwa Afrika yenye ukomavu wa demokrasia, Zambia imeongozwa na marais saba na mmoja ambae alikaimu.

Kwanza, ilianza na Kenneth Kaunda, aliyependwa kwa jina la KK, ambae alikuwa rais wa kwanza wa Zambia baada ya uhuru Oktoba 24, 1964.

Alikuwa kiongozi katika mapambano ya kutafutua uhuru, Kaunda aliongoza nchi hiyo kwa miaka 27 chini ya utawala wa chama kimoja.

Alisimamia elimu, umoja wa kitaifa, na kuunga mkono harakati za mapambano ya uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwaka 1991, Kaunda alikubali kushindwa na upinzani, na kuonesha mfano wa demokrasia kwa kuachia madaraka kwa amani. Alifariki mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 97.

Mrithi wake, Frederick Chiluba, alikuwa ni kiongozi wa umoja wa chama cha biashara ambae alishinda uchaguzi wa mwaka 1991 na kutumikia awamu mbili.

Katika uongozi wake wa miaka kumi, Zambia ilijumuisha mfumo wa vyama vingi na kuinua uchumi. Chiluba alifariki mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 68.

Afariki madarakani

Mwaka 2002, Levy Mwanawasa alikuwa rais wa tatu wa Zambia baada ya kushinda uchaguzi, huku utawala wake ukiendeleza kampeni kabambe dhidi ya rushwa.

Uongozi wake ulikatishwa ghafla na kifo chake mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kupata ugonjwa wa kupooza mwaka mmoja tu baada ya muhula wake wa pili.

Makamu wa Rais Rupiah Banda alikaimu ofisi baada ya kifo cha Mwanawasa na baadae kushinda uchaguzi wa urais mwaka huo. Utawala wake uliwekeza zaidi katika ukuaji wa uchumi hasa kilimo na sekta ya madini.

Mwaka 2011, mwanasiasa wa upinzani Michael Sata, aliyepewa jina la "King Cobra" kwa matamshi yake makali, alimshinda mgombea aliye madarakani Banda baada ya kushindwa mara tatu.

Sata alileta mabadiliko makubwa katika miradi ya miundombinu, hasa ujenzi wa barabara, na sera za wafanyakazi. Urais wake uliisha ghafla alipofariki akiwa ofisini mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 76.

Halafu Makamu wake, Guy Scott, akakaimu nafasi yake. Scott, aliyefariki Julai 15, 2026 akiwa na umri wa miaka 82, alisimamia uchaguzi wa nchi hiyo mapema mwa 2015.

Uongozi wa Lungu

Edgar Lungu kutoka upinzania alishinda uchaguzi, na utawala wake ulipanua zaidi miundombinu lakini kushuhudia ongezeko la deni la taifa. Alifariki mwaka 2025 akiwa na umri wa miaka 68, miaka minne baada ya kuondoka ofisini.

Rais wa sasa Hakainde Hichilema aliingia madarakani 2021 baada ya kumshinda Lungu aliyekua madarakani.

Uongozi wa Hichilema umeweka kipaombele zaidi katika ulipaji wa deni la taifa, na kukuza uchumi, elimu ya bure, na mabadiliko katika kupambana na rushwa.

Umaarufu wake utajaribiwa katika uchaguzi unaokuja ambapo anakabiliwa na wagombea kadhaa kutoka upinzani, Brian Mundubile kutoka Tonse Alliance akiwa mpinzani wake mkuu.