Uwanja wa Ndege wa Ghana: Kutoka Kotoka hadi Accra
Baada ya miaka 60 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ghana unabadilishwa jina kutoka ulivyojulikana kwanza Kotoka hadi Accra.
Jina la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ghana katika mji linbadilishwa, sababu? Jina la awali ni la kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Emmanuel Kwasi Kotoka ambaye alikuwa
madarakani kwa chini ya mwaka mmoja na ndiye aliyempindua Baba wa Taifa hilo Francis Kwame Nkrumah 1966, maarufu Osagyefo lenye maana ya ‘’anayeokoa’’.
Emmanuel Kotoka mwenyewe aliuawa sehemu iliopo uwanja wa ndege na ndipo miaka miwili baada ya kifo chake jina likabadilishwa ili kumuenzi.
Waziri wa Uchukuzi Joseph Bukari Nikpe amenukuliwa akisema kuwa mabadiliko ya jina ni kutoa taswira ya kutoegemea upande wowote na kulipa hadhi jina la mji mkuu wa nchi, Accra.
Kuna wale ambao wamekuwa wakipinga kubadilishwa kwa jina hilo kama kiongozi wa walio wachache bungeni Alexander Afenyo-Markin anayesema itakuwa ni usaliti kwa watu wa kanda ya Volta, anakotoka Kotoka.
Anadai jina hilo ni miongoni mwa maeneo machache yaliyokuwa yanawapa hadhi watu wa kanda ya mashariki.
Katika taarifa mapema wiki hii mamlaka zinasema kubadilishwa kwa jina hakutaathiri shughuli za uwanja wa ndege, viwango vya usalama au usafiri wa kimataifa.
Je, kumuenzi mtu ni lazima maeneo muhimu yapewe jina lake au kukumbuka mchango wake inatosha?