Wakazi wa eneo hilo walisema washambuliaji hao waliwalenga vijana waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu.
Gavana Ahmadu Umaru Fintiri amethibitisha kuwa watu wasiopungua 29 waliuawa katika shambulio la kikatili kautoka jamii ya Guyaku, katika Eneo la Serikali ya Mtaa la Gombi,” msaidizi wake aliandika katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii.
ZILIZOPENDEKEZWA
Mkazi mmoja wa eneo hilo, Philip Agabus, aliliambia shirika la habri la AFP kwamba shambulio hilo lilitokea Jumapili mchana wakati “watu wetu walipokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mpira wa miguu kutoka jamii ya Guyaku… walishambuliwa na wahalifu waliokuja wakiwa na silaha na kuanza kufyatua risasi ovyo.”
CHANZO:AFP



















