Mke wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, Emine Erdoğan, amesema kuwa kuna uwezekano wa kutatua matatizo ya nyakati hizi kupitia njia shirikishi.
Emine Erdoğan alituma ujumbe kwa njia ya video, kwenye jukwaa la 6 la Mkutano wa Viongozi Wanawake, uliofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi chini ya uenyeji wa Angeline Ndayishimiye, mke wa rais wa nchi hiyo, Evariste Ndayishimiye.
Akiutakia mkutano huo heri na fanaka, Emine Erdoğan alibainisha kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na idadi kubwa ya vijana, na watoto wapatao bilioni 2, wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19.
Akisisitizia jukumu lililo mbele kwa sasa, Emine Erdoğan alisema kuwa fursa mbalimbali zikiwemo zile za kielimu na mazingira salama ya kuishi, huakisi mustakabali wa maisha.
“Wakati baadhi ya watoto wakishuhudiwa kuminywa kwa fursa, wapo wengine wanaokosa kabisa hata haki zao za kimsingi,” alisema.
Akionesha hali ya matabaka kwa sasa ulimwenguni, Emine Erdoğan alisema:
“Kwa upande mmoja, maisha ya watoto ni ya kushtua. Uraibu mbalimbali kama vile mitandao ya kijamii na michezo ya video imeathiri makuzi yao. Kwa upande mwingine, zaidi ya watoto bilioni moja hawana fursa za intaneti kwa ajili ya kujipatia elimu. Wakati wengine hula milo yao yenye kuhusisha vyakula vili zindikwa na kukabiliwa na tabia ubwete, huku watoto milioni 181 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Licha ya familia kuwa taasisi muhimu ya makuzi ya mtoto, zaidi ya watoto milioni 140 wamegeuka kuwa wakiwa.”
Kulingana na Emine Erdoğan, kuna hatari kubwa zenye kuwakabili vijana, akisema kuwa kuwa wakati ambapo masuala mbalimbali kama uonevu na unyanyasaji umezua mijadala, ambapo leo masuala mbalimbali kama vile mabadiliko ya tabia nchi, majanga, uhamaji, na uharibifu wa mazingira umezalisha misamiati mipya kwenye fasihi ya afya ya akili.
“Utatuzi wa matatizo haya unawezekana kupitia njia mbalimbali shirikishi.”
Emine Erdoğan alisema kuwa kukosekana kwa udhibiti wa masuala ya kidijiti unazalisha changamoto nyingi na kuongeza:
“Teknolojia inazidi kukua kwa kasi, huku nafasi ya maadili ikizidi kupungua ndani ya mifumo ya elimu. Changamoto hizi zinazidi kuwa ngumu na zenye kufanana na utatuzi wake unahitaji ushirikishwaji wa pamoja. Ni muhimu kuondoa changamoto za kimazingira na za kiuchumi. Vile vile, kuwa na kizazi chenye siha njema hakuhitaji umalizwaji wa njaa tu; ila kilimo cha kisasa mageuzi kwenye mtindo wetu wa ulaji. Binafsi, naamini hatua ya kwanza ya mageuzi haya ni uanzishwaji wa ushirikiano imara ambapo familia, shule na jamii zinashirikia pamoja.”
Emine Erdoğan alionesha matumaini kuwa jukwaa hilo litafungua fursa mpya kwa ajili ya maisha ya binadamu, akituma salamu kwa Angeline Ndayishimiye, mke wa rais wa Burundi kutokana na jiithada zake kwa niaba ya watoto.
Kwa upande wake, Angeline Ndayishimiye alitoa shukrani zake kwa Emine Erdoğan kwa kushiriki kwenye jukwaa hilo kupitia ujumbe wa video.
“Ninamshukuru na kumpongeza Mama Angeline Ndayishimiye Ndayubaha, mke wa rais wa Burundi kwa kuongoza jitihada hizi muhimu.”



















