Trump: Marekeni yafikiria 'kupunguza" operesheni ya kijeshi Iran

Trump amesema mataifa maengine yanayotumia Mlango Bahari wa Hormuz waulinde, sio Marekani.

By
Trump amesema Marekani inafikiria kupunguza operesheni ya kijeshi Iran. / TRT Afrika Swahili

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Ijumaa kuwa anafikiria "kupunguza" operesheni ya kijeshi dhidi ya Iran na kwamba Mlango Bahari wa Hormuz utahitaji "kulindwa" na nchi nyengine ambazo zinautumia.

"Tunakaribia kufikia malengo yetu na tunafikiria kupunguza operesheni zetu za kijeshi Mashariki ya Kati hasa kwa Utawala wa Kigaidi wa Iran," Trump aliandika katika mtandao wa Truth Social.

"Mlango Bahari wa Hormuz utalindwa, na mataifa mengine yanayoutumia-- Marekani haiutumii!" amesema.

Hali ya wasiwasi ya kikanda imeibuka tangu Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran Februari 28.

Mashambulizi hayo yanaripotiwa kuuwa takriban watu 1,300, ikiwemo zaidi ya watoto 150 katika shule ya wasichana.

Iran imejibu kwa kulipiza kisasa kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani kwa kuilenga Israel na kile inachosema miundombinu yenye uhusiano na Marekani katika eneo hilo, hivyo kuongeza mgogoro huo.