Rais Museveni wa Uganda azindua kampuni ya kwanza ya bima ya Kiislamu
Rais Museveni wa Uganda amewataka wananchi kutumia fursa ya mikopo bila riba kwa ajili ya uzalishaji na sio kwa matumizi.
Rais Museveni amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kwa ajili ya uzalishaji. / TRT Afrika Swahili
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezindua kampuni ya kwanza ya bima ya Kiislamu nchini humo iitwayo Tamini General Insurance.
Tamini inaendesha mfano wa kusaidiana, kukopa bila riba na kugawana hatari, kwa ushirikiano na benki ya Kiislamu nchini iitwayo Salaam Bank.
Rais Museveni alisema, "Hili si jambo geni, ni njia yetu ya kitamaduni. Kopeni, lakini kopeni kwa ajili ya uzalishaji, si kwa matumizi. Bima hii pia itafikiwa watu wa kipato cha chini, jambo ambalo ni muhimu sana."