Mahakama ya kimataifa ya upatanishi imekataa ombi la mamilioni ya dola la Rwanda dhidi ta Uingereza linalohusiana na kuwachukuwa wakimbizi wanaoomba hifadhi ya kisiasa, mkataba ambao Waziri Mkuu Keir Starmer aliufuta mara moja alipoingia madarakani 2024.
Mkataba huo, uliosainia 2022 na mtangulizi wake Starmer, Rishi Sunak, ulijumuisha kuwapeleka wahamiaji wanaoingia Uingereza kwa kutumia mashua katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Walikubaliana kuwalipa Rwanda kugharamia wahamiaji hao.
Waziri wa mambo ya ndani wa Starmer wakati huo Yvette Cooper aliufuta mkataba huo, akiutaja kuwa “ufujaji mkubwa wa fedha za umma kuwahi kutokea.”
Mahakama ya Upatanishi ilikataa madai mawili ya Rwanda, ya pauni milioni 50 kila mmoja (Dola milioni 67), kutokana na kufutwa kwa makubaliano hayo. Tarehe ya maamuzi hayo ni Mei 15, lakini ilitangazwa rasmi na mahakama hiyo ya the Hague siku ya Jumatatu.
Mabadiliko muhimu
Katika uamuzi wa kurasa 76, majaji walisema kuwa mawasiliano ya kidiplomasia ya hivi karibuni wa maandishi kati ya nchi hizo mbili baada ya Starmer kufuta mkataba ni ishara ya makubaliano kuwa Uingereza haitolipa pauni milioni 50 mara mbili, iliotakiwa kulipa Aprili 2025 na 2026, kwa gharama ya wahamiaji kupelekwa nchini humo.
Chini ya makubaliano hayo, wahamiaji walikuwa wapelekwe Rwanda, ambapo madai yao ya kuomba hifadhi yatashughulikiwa na, kama watafanikiwa, watakaa huko. Mahakama ya Juu ya Uingereza iliamua kuwa mkataba huo ni batili na Rwanda siyo nchi ya tatu salama ambapo wahamiaji wanatakiwa kupelekwa huko.
Uingereza inasema katika taarifa: “Uingereza ilitetea msimamo wake, na sasa mahakama imetoa uamuzi katika maeneo yote uliowaridhisha Uingereza."
Rwanda haikutoa taarifa yoyote kuhusu suala hilo mara moja.














