Moja ya maeneo makubwa na maarufu zaidi Afrika Kusini, ni Hifadhi ya Taifa ya Kruger, imeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.
Hifadhi hii ina takriban hekta milioni 2 kwenye mpaka wa kaskazini-mashariki na Msumbiji na hutumika kama msingi wa utalii wa kiikolojia wa kimataifa.
Takwimu kutoka Hifadhi za Taifa za Afrika Kusini (SANPARKS) zinaonyesha kuwa Hifadhi hiyo inalinda mamalia 248, ndege 505, na aina 118 za reptilia, pamoja na takriban aina 2,000 za mimea na miti.
Pia kuna spishi nyengine zilizo hatarini kama vile mbwa mwitu wa Kiafrika, duma, twiga na pundamilia.
Hifadhi hii huvutia idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje, hivyo kukuza sekta ya utalii ya Afrika Kusini na uchumi mpana kupitia mtandao wake mpana wa kutoa huduma ikiwemo nyumba za kulala wageni, kambi na njia za safari.
Ilianzishwa mwaka 1926 chini ya Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya Afrika Kusini, na ni ya kwanza kitaifa nchini humo na moja ya hifadhi kubwa barani Afrika.
Kwa mara ya kwanza maeneo ya hifadhi yalikuwa chini ya ulinzi wa serikali ya Afrika Kusini mwaka 1898, na kuwa Hifadhi ya kwanza ya Taifa nchini humo mwaka 1926.
Hifadhi hiyo hivi sasa inakabiliana na changamoto ambazo ni pamoja na kupunguza ujangili, kudhibiti idadi ya tembo wanaovimba, kushughulikia msongamano katika Hifadhi, kuvutia wageni, na kushughulikia migogoro ya binadamu na wanyamapori.
Pia imekuwa mwathirika wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Januari mwaka 2026, baadhi ya wanyama katika hifadhi hiyo, waliathiriwa na mafuriko na Hifadhi hiyo kufungwa kwa siku kadhaa, na wageni na wafanyakazi waliokwama wakahamishwa kwa kutumia helikopta.
Hata hivyo, licha ya changamoto hizo, Hifadhi ya Taifa ya Kruger bado inaibuka kinara Afrika Kusini na imeaminika kuwa ni miongoni mwa sehemu maridhawa kabisa za kufanya utalii.



















