| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Tebboune athibitisha Algeria kuunga mkono Niger huku kukiwa na tishio la usalama
Ndege nne za kijeshi za Algeria zimefika mjini Niamey huku vikosi vya usalama vya Niger vikichukua udhibiti wa maeneo ya kimkakati yaliyoshambuliwa katika mji mkuu.
Tebboune athibitisha Algeria kuunga mkono Niger huku kukiwa na tishio la usalama
Rais Abdelmadjid Tebounne amesisitiza kumuunga mkono Rais wa Niger Abdourahamane Tiani wa Algeria 'kwa mazingira yoyote.'

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune siku ya Jumatatu alithibitisha taifa lake kuunga mkono Niger, watu wake na taasisi kufuatia jaribio la kutatiza taifa hilo la Afrika Magharibi.

Tebboune aliyasema hayo katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Niger Abdourahamane Tiani kujadili hali ilivyo nchini humo, kulingana na taarifa kutoka kwa ofisi ya rais wa Algeria.

“Rais amemthibitishia ndugu yake Abdourahamane Tiani kuwa Algeria lazima tuwalinde ndugu zetu wa Niger, watu wake na taasisi na kuwaunga mkono katika maeneo yake na mazingira yoyote,” taarifa ilisema.

Tebboune pia alimpongeza Tiani kwa juhudi zake “za kutibua jaribio la kutatiza Niger.”

‘Hali sasa imedhibitiwa’

Kwa upande wake,Tiani, amemuhakikishia Tebboune kuwa “hali sasa imedhibitiwa” na kuwashukuru Algeria kwa kuwaunga mkono Niger na watu wake, kulingana na taarifa.

Siku ya Jumapili, Wizara ya Ulinzi ya Algeria ilitangaza kuwa ndege nne za kijeshi za Algeria zimewasili Niamey “kwa lengo la kuunga mkono jeshi la Niger katika kukabiliana na jaribio la kutatiza nchi.”

Matukio ya hivi majuzi ikiwemo mashambulizi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani na Uwanja wa Jeshi 101, eneo la kijeshi la kimkakati mjini Niamey, pamoja na maeneo mengine ya mji mkuu.

Waziri wa ulinzi wa Niger anasema mashambulizi ya kijeshi mjini Niamey yamedhibitiwa na vikosi vya usalama vimedhibiti hali katika maeneo ambayo yamelengwa.

CHANZO:َAA