Uturuki na Saudi Arabia kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na uwekezaji katika ndege za kivita za KAAN
Uturuki na Saudi Arabi zatia saini makubaliano 'muhimu' ya ushirikiano wa sekta ya ulinzi huku Rais wa Uturuki Erdogan akieleza azma ya Uturuki ya kupanua mikataba hiyo.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa Uturuki na Saudi Arabia zitaimarisha ushirikiano wao katika sekta ya ulinzi, alipokuwa akirudi kutoka mji Mkuu wa Misri, Cairo siku ya Jumatano, akibainisha kuwa ndege ya kivita ya KAAN iliyotengenezwa na nchi yake imesifiwa.
“Tumepokea maoni mengi chanya kuhusu KAAN. Kuna uwekezaji wa pamoja na Saudi Arabia katika eneo hili, na tunaweza kutekeleza ushirikiano huu wakati wowote,” Erdogan aliwaambia waandishi wa habari.
Erdogan alisisitiza kuwa nchi hizo mbili zimesaini makubaliano “makubwa” ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi, akionyesha azma ya Uturuki ya kuyapanua.
Kuhusu mvutano unaoendelea kati ya Iran na Marekani, Erdogan alionyesha matumaini kuwa mvutano huo utaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo, akisisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa mazungumzo.
Kuhusu hali ya Ghaza, Rais wa Uturuki alisema nchi yake itachukua jukumu la moja kwa moja kuhakikisha mpango wa amani wa Ghaza unatekelezwa “vema” na kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo.