Netanyahu: Tumeshambulia reli na madaraja ya Iran

Katika taarifa yake, jeshi la Israel limesema kuwa limeshambulia madaraja 8 yaliyokuwa yakitumika na utawala wa Iran wakati wa kusafirisha zana za kivita".

By
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu./Picha:Reuters

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake imefanya mashambulizi kwenye madaraja na njia za treni zinazotumika na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC).

"Tunaendelea kuumaliza utawala wa kigaidi wa Iran…kwa ari mpya na nguvu mpya,” alisema Netanyahu kwa njia ya picha mjongeo iliyotolewa na ofisi yake.

"Siku ya jana, marubani wetu waliharibu miondombinu ya uwanja wa ndege na helikopta katika kikosi cha anga cha Iran.

Leo hii tumefanikiwa kushambulia reli na madaraja yanayotumika na IRGC."

Katika taarifa yake, jeshi la Israel limesema kuwa limeshambulia madaraja 8 yaliyokuwa yakitumika na utawala wa Iran wakati wa kusafirisha zana za kivita".

Kulingana na msemaji wa jeshi la Israel Brigedia Jenerali Effie Defrin, marubani wa kivita wanaendelea “kuusambaratisha” utawala wa kigaidi wa Iran ".