Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo Makosso ajiuzulu

Kujiuzulu kwa Anatole Collinet Makosso kunakuja siku chache baada ya kuapishwa kwa Rais Denis Sassou Nguesso kwa muhula wa tano.

By
Makosso aliteuliwa 2021. / AA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo Anatole Collinet Makosso amejiuzulu yeye pamoja na Baraza lake la Mawaziri, kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali mpya, ofisi ya rais ilisema katika taarifa siku ya Jumapili.

Hatua hii inakuja baada ya kuapishwa kwa Rais Denis Sassou Nguesso kwa muhula wa tano kufuatia uchaguzi wa Machi 15 katika taifa hilo la Afrika ya Kati, ambalo pia linafahamika kama Congo-Brazzaville.

Wakati wakisubiri kuundwa kwa serikali mpya, mawaziri wanaoondoka wataendelea na majukumu ya kuratibu masuala ya serikali, taarifa ilisema.

Makosso, ambaye aliteuliwa 2021, “alitia shukrani zake kwa Kiongozi wa Nchi kwa kumuamini na jukumu hilo na kueleza kuwa yuko tayari kutumikia nafasi yoyote ile ambayo itampendeza Rais wa Jamhuri.”

Kutatua migogoro

Wakati wa hafla ya kuapishwa wiki iliopita, Nguesso aliahidi “kuchangia katika kutatua migogoro ambayo inarudisha nyuma bara la Afrika.”

Nguesso alipata kura karibu asilimia 95%. Wagombea wengine sita walikuwa wanashindana na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kuongoza taifa hilo la Afrika ya Kati ambalo lina moja ya hifadhi kubwa ya mafuta kuini mwa Jangwa la Sahara.

Sassou Nguesso ni rais wa tatu barani Afrika ambaye amekuwa uongozini kwa muda mrefu, wa kwanza akiwa wa Paul Biya wa Cameroon na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea.

Kura ya maamuzi ya katiba 2015 iliondoka ukomo wa umri na muhula wa urais, kumpa fursa Nguesso kugombea tena.