CCM yaadhimisha miaka 49 tangu kuanzishwa

Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania chaadhimisha miaka 49 tangu kuanzishwa kwake.

By
Wafuasi wa CCM waadhimisha miaka 49 tangu kuanzishwa kwa chama hicho katika maeneo kadhaa nchini Tanzania. /CCM/ / Facebook

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, amehudhuria maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Februari 5, 2026 katika Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa wanachama wa CCM kutekeleza wajibu wao wa msingi na wa kudumu kwa kuhakikisha chama kinaendelea kuwa cha Watanzania wote na kuwa ndio kimbilio lao.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa kila mwanachama na kiongozi wa CCM anatakiwa kutafakari matendo yake na namna yanavyochangia maendeleo, kuimarisha umoja na mshikamano wa chama pamoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Nchimbi amesema kuwa wakati chama kikielekea katika uchaguzi wa ndani kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa mwaka 2027, ni muhimu kwa wanachama kuanza kujiandaa mapema kwa kuzingatia misingi muhimu ikiwemo kulinda maadili ya chama, kudumisha umoja na mshikamano, kuendeleza amani na utulivu, pamoja na kutambua kuwa uongozi ni dhamana ya kuwatumikia wananchi.