| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan aapa kuipigania dola ya Kipalestina
Kulingana na Erdogan, Uturuki itaendelea kuhakikisha kuwa Yerusalemu Mashariki, inakuwa mji mkuu wa Palestina, kulingana na makubaliano ya mwaka 1967.
Erdogan aapa kuipigania dola ya Kipalestina
Erdogan alisema kuwa Uturuki inapingana vikali na uchokozi wenye kulenga kubadilisha nafasi ya msikiti wa Al -Aqsa Mosque na nyumba zingine za ibada k

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake itaendelea kupambania kupatikana kwa dola ya Kipalestina.

Rais Erdogan, ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, uliofanyika siku ya Jumatano jijini Ankara.

Kulingana na Erdogan, Uturuki itaendelea kuhakikisha kuwa Yerusalemu Mashariki, unakuwa mji mkuu wa Palestina, kuligana na makubaliano ya mwaka 1967.

Erdogan aliituhumu serikali ya Benjamin Netanyahu, kwa kujaribu kuiondoa Palestina kwenye ajenda ya dunia.

"Serikali ya Netanyahu inajaribu kuifuta Palestina kutoka kwenye ajenda ya dunia, kwa kuendelea kufaidika na mgogoro katika kanda hiyo, hawatofanikiwa katika hilo,” alisema.

Erdogan atahadharisha kuhusu miji mitakatifu ya Yerusalemu

Erdogan alisema kuwa Uturuki inapingana vikali na uchokozi wenye kulenga kubadilisha nafasi ya msikiti wa Al -Aqsa Mosque na nyumba zingine za ibada katika eneo la Yerusalemu Mashariki.

Wakati huo huo, aliilaumu Israel kwa kuendelea na vitendo vyake vya kidhalimu katika eneo la Ukingo wa Magharibi na Yerusalemu Mashariki.

 “Tuna wajibu wa kuisaidia Palestina, hususani kwa Waislamu wote,” alisema Erdogan.

Palestina yaupongeza mkataba wa Mecca

Hali kadhalika, Erdogan alisisitizia umuhimu wa kuanzishwa kwa mchakato wa ujenzi mpya wa Gaza kuhakikisha usalama wa eneo hilo.

Kulingana na Erdogan, Uturuki itaendelea na jitihada zake za kuwaunga mkono Wapalestina na kutetea haki zao.

Abbas alikuwa jijini Ankara kwa ziara ya kikazi, wakati ambapo Uturuki inaendelea na michakato ya kidiplomasia na Palestina, kuhusiana na mustakabali wa Gaza.

Kwa upande wake, Abbas alipongeza mkataba wa pamoja wa ulinzi wa Mecca, akiuelezea kuwa hatua muhimu ya kutafuta utulivu wa kikanda.

Pia, alimshukuru Erdogan kwa kuendelea kuiunga mkono Palestina na harakati za kujikomboa.

CHANZO:TRT World and Agencies