Rwanda yaishtaki Uingereza kwa kukiuka makubaliano ya mkataba wa uhamishaji wa wakimbizi
Rwanda imeishtaki Uingereza kwa kuvunja masharti ya mkataba katika 'kipengele cha malipo ya kifedha'
Rwanda imeifungulia mashtaka serikali ya Uingereza kufuatia makubaliano tata ya uhamiaji ambayo Uingereza imeachana nayo miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer aliachana na mpango huo kati ya nchi mbili hizo, ambao ulianzishwa na serikali iliyopita ya Uingereza, punde tu baada ya kuingia madarakani Julai 2024, hasa baada ya kufuatia upinzani mkali kutoka vya wanaharakati.
Imeripotiwa kwamba Uingereza imeilipa Rwanda kiasi cha paundi milioni 240 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani milioni 330.9 kabla ya kusitishwa kwa makubaliano hayo.
Mwezi Novemba 2024, Uingereza iliiomba Rwanda kuachana na awamu mbili za malipo ya pauni milioni 50 ambayo yalitakiwa kulipwa kati ya Aprili 2025 na Aprili 2026, kwa madai kwamba inafanya hivyo ikitarajia kusitisha makubaliano hayo, kwa mujibu wa Rwanda.
Makubaliano mapya
Rwanda iliashiria kukubali utaratibu huo iwapo makubaliano hayo yatasitishwa, ikizingatiwa kwamba makubaliano mapya ya malipo yatajadiliwa na kuafikiwa.
Lakini majadiliano kati ya Rwanda na Uingereza hayakufanyika, na “muda wa malipo umefika kwa makubaliano ya zamani," imesema taarifa hiyo.
Rwanda, imepeleka kesi katika Mahakama ya Upatanishi Uholanzi Novemba mwishoni baada ya Uingereza kuweka wazi kwamba haina nia ya kuendelea kulipa chini ya makubaliano hayo.
Katika taarifa yake, Rwanda inamtuhumu Waziri Mkuu wa Uingereza kwa kutangaza kuwa "makubaliano hayo yamekufa na kuzikwa" bila kutoa taarifa kwa Rwanda, kinyume na ari ya ushirikiano uliyopo.
Pia inaituhumu Uingereza kwa kukiuka makubaliano "ya utaratibu wa malipo" pamoja na "kukataa kufanya utaratibu wa kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda."
“Rwanda inasitishwa kwamba imelazimika kupeleka madai haya mahakamani, lakini baada ya Uingereza kuonesha kutojali, imekosa namna," imeongeza taarifa.
Uingereza iliingia mkataba tata wa uhamiaji na Rwanda Aprili 2022 ambao umewezesha wahamiaji wanaofika Uingereza kupelekwa nchini Rwanda, ambapo madai yao ya kuomba hifadhi yangeshughulikiwa.
Lakini alipoingia madarakani, Starmer alitangaza kutoendelea na mpango huo ulioanzishwa na serikali iliyokuwa madarakani, na kusema "haungeweza kusaidia kupunguza uhamiaji.