Makala ya saba ya tuzo za TRT World imelighubikwa na hisia baada ya Mke wa rais wa Uturuki, Emine Erdogan kumkumbatia mama mzazi wa mwandishi wa Gaza Yahya Barzaq.
Tuzo hizo ziliwatambua walimu, wahandisi, wana mawasiliano na kada zingine ambazo zilichangia kwenye ustawi wa watu kwenye jamii.
Kati ya waliohudhuria, ni pamoja na Mke wa rais wa Uturuki Emine Erdogan ambaye alioneshwa kufurahishwa na tukio hilo.
Kupitia ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa X, Mke huyo wa rais alisisitiza kuwa, tukio hilo ni ukumbusho kuwa, ubinadamu hautambui mipaka, na kuwa mashujaa wasioimbwa wanaendelea kupigania haki ulimwenguni.
Tuzo ya muelimishaji kwa mwaka huu ilienda kwa Rudayna Abdo, ambaye ni muasisi wa jukwaa la Thaki, ambaye kupitia teknolojia, amewawezesha maelfu ya wakimbizi wa Lebanon na Jordan kupata elimu bora.
Kwa upande mwingine, tuzo ya vijana ilikwenda kwa mwanaharakati wa Nigeria Amara Nwuneli, kwa kutambua mchango wake katika kugeuza sehemu za kutupia taka kuwa viwanja vya kuchezea.
Tuzo ya mawasiliano ilikwenda kwa Ibtihal Abousaad na Vaniya Agrawal, kutambua suala la maadili katika ulimwengu wa Akili Mnemba.
Yahya Barzaq
Kisha ikaja tuzo kubwa kwa usiku huo, ambayo ilitolewa kwa Yahya Barzaq, mwanahabari aliyeuwawa Gaza.
Barzaq aliuwawa Septemba 30, katika shambulio la Israeli, wakati akiripoti kutoka Gaza.
Katika risala yake, Emine Erdogan alimkumbuka Barzaq na Wapalestina wote waliouwawa na Israel.
Alimuelezea Barzaq kama ndugu aliyeuwawa kwa kuonesha ulimwengu uhalisia wa yanayoendelea Gaza.
Alitumia fursa hiyo kumuombea mwanahabari na Wapalestina wote.
Wakati wa hisia
Hisia ilitawala wakati Emine Erdogan alipomkumbatia mama mzazi wa Yahya Barzaq.
Tuzo ya Ujumla ilienda kwa mhandisi wa Kiitaliano Raul Pantaleo, ambaye kazi yake iliwezesha upatikanaji wa huduma za afya.
Akizungumzia kazi ya kila mshindi wa tuzo, Emine Erdogan alisema kuwa hizo zimedhihirisha kuwa ubinadamu bado unaendelea ulimwenguni.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza washindi wa tuzo hizo kwa ujasiri wao.
Pia aliishukuru familia ya TRT kwa maandalizi ya tukio hilo.














