Kampuni ya Boeing kulipa zaidi ya dola milioni 28 kwa familia ya aliyefariki katika ajali ya ndege

Kama idadi kubwa ya abiria wengine katika ndege hiyo iliyoanguka, Garg, mshauri wa Mipango ya Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, alikuwa akielekea kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira huko Nairobi, Kenya.

By
Ndege ya Boeing ilianguka Ethiopia Machi 2018

Mahakama ya Marekani imeamuru zaidi ya dola milioni 28 ipewe familia ya mshauri wa Umoja wa Mataifa aliyefariki katika ajali ya ndege aina ya Boeing 737 Max nchini Ethiopia zaidi ya miaka sita iliyopita.

Uamuzi huo ulifikiwa Jumatano kwa niaba ya jamaa wa Shikha Garg baada ya saa mbili ya mashauriano ya jopo la wazee wa mahakama (jury) ambayo yalimaliza kesi ya wiki moja huko Chicago, ambapo Boeing ilikuwa na makao yake makuu.

Kama idadi kubwa ya abiria wengine katika ndege hiyo iliyoanguka, Garg, mshauri wa Mipango ya Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, alikuwa akielekea kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mazingira huko Nairobi, Kenya.

Ilikuwa ni kesi ya kwanza kwa mtu kudai fidia iliyotokana na ajali ya Machi 2019 ambayo watu wote 157 waliuawa katika ndege ya Ethiopian Airlines 302.

"Sisi na familia tumeridhishwa na uamuzi wa mahakama. Inaelekeza uwajibikaji kwa umma kwa mwenendo mbaya wa Boeing," mawakili wa familia hiyo, Shanin Specter na Elizabeth Crawford, walisema katika taarifa baada ya hukumu hiyo kusomwa mahakamani.

Boeing italipa dola milioni 3.45 za ziada kwa mume wa Garg, Soumya Bhattacharya, kama sehemu ya makubaliano kati yake na kampuni iliyofikiwa nje ya mahakama.

Hiyo, pamoja na malipo ya riba ya 26%, itakuwa jumla ya kiasi ambacho Boeing italipa kwa familia ya Garg hadi $ 35.8 milioni.

Kampuni hiyo ya ndege imejadiliana kuhusu suluhu badala ya kesi mahakamani katika kesi nyingi za vifo zilizowasilishwa kuhusiana na ajali hiyo na nyingine kama hizo ya 737 Max miezi mitano kabla katika pwani ya Indonesia, ingawa maelezo ya makubaliano hayo yalikuwa ya siri na hayakufichuliwa.

Wanasheria wanasema kesi zisizopungua kumi na mbili bado hazijatatuliwa.

Katika taarifa Jumatano, Boeing iliomba msamaha kwa familia zote za waathiriwa na kusema inaheshimu haki yao ya kuwasilisha madai yao mahakamani.